Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FIFA YATOA RUKSA SUAREZ KUFANYA MAZOEZI

 

FIFA imesema Luis Suarez ataruhusiwa kufanya mazoezi na Liverpool wakati akitumikia adhabu yake ya miezi minne na mechi nane za kimataifa. 
Wakati huohuo Uruguay imekata rufaa kupinga adhabu hiyo.
Suarez alifungiwa
"shughuli zote zinazohusu kandanda" baada ya kumng'ata Georgio Chiellini wa Italy. 
Hata hivyo Claudio Sulser, mkuu wa kamati ya nidhamu ya FIFA alipoulizwa siku ya Alhamisi mjini Rio de Janeiro kuhusu adhabu hiyo alisema:
 Hapana huwezi kumnyima haki hiyo mchezaji, kwa sababu haitakuwa sawa.
Sulser pia amethibitisha kuwa Uruguay imekata rufaa kupinga adhabu iliyotolewa. 
Claudio Sulser pia amesema Suarez ambaye anasakwa na Barcelona, ataruhusiwa kuhusika katika mchakato wa uhamisho.
 Mchezaji haruhusiwi kujihusisha na chochote kuhusu kandanda, lakini vipimo vya afya vinaruhusiwa. Adhabu hii haihusiki na haki ya kuhama timu
amesema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top