Luiz Felipe Scolari, kocha wa Brazil
*****
“Ni wakati mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na siku mbaya zaidi katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea. Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.

Lilikuwa chaguo langu.
Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo, tulicheza kwa kiwango chetu cha
mwisho-lakini tumeishia dhidi ya timu kubwa ya Ujerumani. Hatukukata
tamaa na kurudi nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada ya kufungwa bao
la kwanza na kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani hawawezi
kuelezea ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na unatakiwa
kuheshimu hilo.
Tunatakiwa kujiunza jinsi ya
kukabiliana nalo. Ujumbe wangu kwa watu wa Brazil ni huu. Tafadhali
watusamehe kwa kiwango hiki. Ninaomba radhi kwasababu hatujaweza kufika
fainali-na tutajitahidi kushinda mechi ya nafasi ya tatu. Bado tuna
sababu ya kucheza.”
Post a Comment