Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA TUKIO LA MAJAMBAZI KUVAMIA GARI LA MAGEREZA NA KUPORA MAHABUSU .... MCHONGO MZIMA WAVUJA ... POLISI WATOA TAMKO

 Wananchi wakiliangalia basi la mahabusu la Jeshi la Magereza namba MT 0046,  ambalo lilishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana na kudaiwa kumpora mahabusu mmoja na kutokomea naye leo katika Barabara ya Old Bagamoyo,  karibu na Mayfair, Mikocheni, Dar es Salaam. Mahabusu wawili walijeruhiwa na askari mmoja wa magereza. 


 sehemu ya nyuma ya basi hilo ikiwa wazi baada kioo kusambaratishwa na kufanikiwa kumpitishia mwenzao

 


 

Kwa mujibu wa mdau aliyeshuhudia tukio lote hilo live anatupasha:
Ishu ilikuwa hivi, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki road.

Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana. Nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.
Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puuu! puuu! pooo! poooo! poooo! kama risasi 6 au 8 hivi - kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote.
Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja.
Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari wake wakaiona hiyo ishu live. Sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa risasi wale askari magereza.

Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwa speed ya 220.
Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu. Yaani ilikuwa kama Movie (ya ulaya, sio Bongo Movie).
*******

KAMANDA WA POLISI KINONDONI AZUNGUMZIA TUKIO LA BASI LA MAGEREZA KUSHAMBULIWA KWA RISASI

Basi la Magereza lililokuwa limebeba wafungwa/maabusu limeshambuliwa kwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi leo (July 2) katika eneo la Mikocheni, Dar es Salaam.Akizungumza leo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camellius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi.Kamanda Wambura amesema ni mapema kutaja nia ya watu hao wenye silaha waliovamia gari hilo kwa kuwa wanaweza kuwa na nia tofauti kabisa na fikra za haraka.

Tunafanya uchunguzi ambao utatufikisha mahali tuweze kubaini ni nini. Inawezekana pengine kuna wahalifu walikuwa katika harakati za uhalifu ghafla wakaona basi lile ambalo lina askari wazuri wenye silaha wakaanza kulishambulia…inawezekana. Au inawezekana vingine vyovyote ambavyo hatuwezi kufikiri wala kubaini.” Kamanda Wambura ameiambia 100.5 Times Fm.
Ameeleza kuwa hakuna maabusu yoyote aliyeweza kutoroka katika tukio hilo na kwamba madhara yaliyotokea kwenye gari hilo sio makubwa. Amesema bado hajapata taarifa yoyote ya uharibifu wa mali au upotevu wa mali uliotokea katika eneo hilo kufuatia tukio hilo.
Akizungumzia watu waliojeruhiwa katika tukio hilo, Kamanda Wambura amewataja watatu waliopata majeraha kuwa ni dereva wa basi hilo, mahabusu mmoja na askari mmoja wa kike.
Kuna baadhi wana michubuko, wale wawili ambao ni dereva na mahabusu mmoja. Lakini kuna askari wa kike ambaye yeye ana majeraha kwenye kifua upande wa kulia. Lakini ni nini kimesababishia michubuko ile hatuwezi kujua kama ni vioo ama ni purukushanai wamejichubua mle ndani au vitu gani.” Amefafanua.
Chanzo: 100.5 Times Fm
 
PICHA NA WADAU WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top