Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LEMBELI ATAKA MADIWANI WAZEMBE KAHAMA WAZOMEWE.


MBUNGE WA KAHAMA MH JAMES LEMBELI
‘Mimi nilivyozomewa mwaka 2010 mbele ya Rais Jakaya Kikwete nilijifunza mengi na leo hii siwezi kuzomewa tena.” James Limbeli 

Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli amewataka wananchi kuwazomea madiwani wazembe wasioleta maendeleo yaliyo ndani ya uwezo wao.
 
Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mayila, Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Lembeli alisema ni haki ya wananchi kuwazomea madiwani wa aina hiyo.

Kauli hiyo ilikuja baada ya wananchi kulalamikia ubovu wa barabara katika mtaa huo, ambao walidai kwa miaka 17 iliyopita, eneo hilo halijawahi kufanyiwa matengenezo ya miundombinu yake.

Alisema pamoja na mambo makubwa aliyofanya diwani wa eneo hilo, Amosi Sipemba, siyo mwisho wa kuleta maendeleo mengine ambayo yapo chini ya halmashauri na kwamba diwani anahudhuria vikao vyote vya uamuzi.

“Suala la barabara ni la diwani wenu, mimi kazi yangu ni kusukuma tu kwa kuwa jimbo langu lina kata 34, hivyo ni vigumu kutambua matatizo ya wananchi bila kupitia kwa diwani. Mwambieni diwani wenu na atanifikishia,” alisema Lembeli na kuongeza:

“Huyu mkimwambia atanifikishia nami, nitakwenda kusukuma huko kwenye halmashauri, mwambieni ikibidi mzomeeni ili akamweleze mke wake alivyozomewa.

Mimi nilivyozomewa mwaka 2010 mbele ya Rais nilijifunza mengi na leo hii siwezi kuzomewa tena.”

Hata hivyo, kabla ya hapo Diwani wa Kata ya Nyihogo, Sipemba alisema tangu aingie madarakani mwaka 2010 hakukuwa na barabara yoyote iliyochongwa katika eneo hilo, lakini hadi sasa asilimia kubwa zimefanyiwa matengenezo.

Akizungumzia kuhusu kuzomewa na wananchi, Sipemba alisema yeye siyo mhandisi wa kutengeneza barabara na kwamba hata yeye pia anaomba kutoka halmashauri ya mji.

SOURCE:MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top