Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANAFUNZI WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA KWA KUKOSA NAFASI KIDATO CHA TANO MKOANI MBEYA

 

WAHITIMU 39 wa kidato cha nne mwaka jana katika Shule ya Sekondari Karobe jijini hapa wakiwa na wazazi wao, jana waliandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kujua hatma yao baada Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa kuwapangia nafasi za kujiunga kidato cha tano licha ya kufanya vizuri katika mitihani yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi hao pamoja na wazazi wao, walisema kuwa waliamua kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kujua hatima yake, baada ya kuona hawapewi majibu ya kuridhisha kutoka kwa viongozi wa chini yake.
Walisema tangu wizara itangaze majina kwa ajili ya kujiunga kidato cha tano wiki mbili zilizopita, wameshangazwa kuona wanafunzi kutoka shule hiyo hawajapangiwa kwa ajili ya kuendelea na masomo katika ngazi hiyo, licha ya kuwa na ufaulu mzuri.
Wanafunzi hao ambao wamepata alama za daraja la kwanza hadi tatu, hawajui hatima yao kutokana na wizara husika kushindwa kuwapangia shule kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
Nao wazazi ambao waliambatana na watoto wao hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (CHADEMA) kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala hilo, walisema kuwa tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina ya wanafunzi waliofaulu kwa ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa, hakuna majina ya watoto wao.
Mmoja wa wazazi hao, Lawrance Shimo, alisema baada ya kufuatilia kwa kina ikiwemo kuuliza uongozi wa shule, walibaini kuwa katika shule hiyo hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa shule kwa ajili ya kuendelea na kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa alama mzuri.
Na Keneth Ngelesi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top