Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Linah Aeleza Kinachoendelea kumuweka Mjini Bila Kuwa Na Nyimbo Mpya Na Shows


Ndege Mnana, Linah ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya bila kuachia wimbo mpya kabla ya kuachia remix ya wimbo wa Kizaizai wa Diamond ameeleza sababu zinazomfanya aendelee kuishi maisha mazuri hata anapokuwa hana wimbo mpya redioni kiasi cha kupunguza mfululizo wa shows.



Linah alifunguka katika Power Jams ya East Africa Radio  jana kuwa sababu kubwa inayomfanya aendelee kung’aa mjini hata bila shows wala kuwa na nyimbo mpya ni kujipanga mapema kuikabili hali yoyote itakayojitokeza kwenye maisha yake kama mwanamuziki. 

 

“Labda niseme kitu kimoja, unajua unapokuwa msanii unatakiwa ujipange vya kutosha. Anything can happen. Kwa hiyo unapofanya kazi at the time unapokuwa vizuri inabidi ujipange kwa maisha ya mbele pia. Kama mimi nilikuwa nimejipanga enough kwamba in case ikitokea kitu chochote mimi niko sawa. Yaani sitatetereka.”



 Amesema anajua msanii anapotetereka anamuangusha shabiki wake anapotaka kujigamba kwa wenzake jinsi anavyomkubali msanii huyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top