Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LULU AWACHANA WABAYA WAKE LIVE


Kumbe! Sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kwamba amewajua wabaya wake wanaomfuatilia na kumsakama kwa ubaya katika maisha yake, amewaonya kuwa dawa yao ipo jikoni.
Sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita jijini Dar, Lulu alisema kuwa kila kukicha lazima watu hao waibuke na jipya linalomhusu yeye, mbaya zaidi ni kwa ajili ya kumchafua.
“Mara utasikia Lulu kagombania bwana, mara Lulu kafanya sijui kitu gani lakini ukiangalia hakuna hata cha ukweli kwa kuwa nimekuwa staa basi kila mtu ana lake la kuongea, kifupi nimeshawajua wabaya wangu na kwamba ni wengi sana, nawaambia niko njiani kuwaandalia dawa yao ambayo naamini itakuja kuwa fundisho kwao na kwa wengine,” alisema Lulu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.
Hii ni mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kufunguka kuhusu suala hilo lakini Ijumaa Wikienda linamuomba asichukue sheria mkononi kwani kibao kinaweza kumgeukia.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top