Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Klaus
Chilima kukagua gwaride maalum la makaribisho kwa Mheshimiwa Makamu wa
Rais wa Tanzania baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Lilongwe
kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi
zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake
Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06, 2014.
Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada ya
shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi
kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni
Mama Asha Bilal.
Wa
pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi
Profesa Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha
Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya
Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika
jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe,
Malawi. Picha na OMR.
********
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
leo Jumapili Julai 06, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika maadhimisho
ya miaka 50 ya Uhuru wa Malawi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa
Civo jijini Lilongwe.
Katika
sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia alihudhuria
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Waziri Mkuu wa Msumbiji na viongozi
mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika.
Sherehe hizo zilianza kwa ibada ya misa asubuhi na kisha kuhamia katika
uwanja wa Civo mchana ambapo Rais wa Malawi Prof. Athur Peter Mutharika alikagua gwaride na kisha kuwasha Mwenye wa Jubilee ya miaka 50 na baadaye kulihutubia taifa.
uwanja wa Civo mchana ambapo Rais wa Malawi Prof. Athur Peter Mutharika alikagua gwaride na kisha kuwasha Mwenye wa Jubilee ya miaka 50 na baadaye kulihutubia taifa.
Akizungumza
katika sherehe hizo, Rais Mutharika alisisitiza kuhusu umuhimu
wananchi wa Malawi kuwa wamoja na akaeleza nia yake ya kujenga umoja
kwa nchi zinazoizunguka Malawi pamoja na zile za Kusini mwa Afrika.
Baada ya hotuba hiyo, sherehe hizo ziliendelea na mchezo wa soka baina
ya timu ya taifa ya Malawi na Msumbiji.
Malawi
ilipata uhuru wake mwaka 1984 ikiongozwa na Rais wake wa kwanza Dkt.
Kamuzu Banda hadi mwaka 1994. Baada ya mwaka huo alifuata Rais Dkt.
Bakili Muluzi aliyetawala kuanzia mwaka 1994 hadi 2004.
Baaada
ya mwaka huo alifuata Rais Profesa Bingu wa Mutharika aliyetawala hadi
mauti yalipomkuta mwaka 2012. Dkt. Joyce Banda aliyekuwa Makamu wa Rais
wa Mutharika alichukua madaraka na kukaa hadi mwaka huu 2014 ambapo
Malawi iliingia katika uchaguzi mkuu na kisha Rais Profesa Arthur Peter
Mutharika aliposhinda uchaguzi huo na hivyo kuwa Rais wa nne wa Malawi.
Katika
sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma
Maalim na Mheshimiwa Makamu wa Rais amerejea nyumbani Tanzania Julai 07,
2014 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai 06, 2014
Julai 06, 2014
Lilongwe: Malawi
Post a Comment