Sori: Mwandishi wetu
MWANAMUZIKI aliyefariki dunia, Amina Ngaluma maarufu kama Japanese alifikisha siku 40 tokea azikwe Jumamosi iliyopita, lakini katika kisomo kilichosomwa nyumbani kwao Kitunda, hakuna staa yoyote wa muziki wa dansi aliyehudhuria.
Japanese alifariki dunia mwezi uliopita nchini Thailand alikokuwa akifanya kazi ya muziki na katika shughuli hiyo ya wiki iliyopita, masheikh mbalimbali walihudhuria kwa kisomo kabla ya kufuturisha watu.
Kabla ya mauti kumfika, Japanese aliwahi kufanya kazi kwa kujituma katika bendi za African Revolution ‘Tam Tam’, Double M Sound na TOT, lakini katika hali ya kusikitisha hakuna hata mwanamuziki mmoja aliyehudhuria zaidi ya mumewe, Rashid Sumuni.

Post a Comment