Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MICHAEL WAMBURA AMTUPIA MADONGO RAIS MPYA WA SIMBA KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI


ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa TFF, Michael Wambura ameishangaa kamati ya utendaji ya Simba ya kupeleka suala lake kwenye mkutano mkuu, wakati sakata lake limeshamalizika na kamati ya rufaa ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Julius Lugaziya.
Wambura ameyasema hayo leo mchana alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari alipowasilisha mada ya kuwatetea wanachama 69 waliosimamishwa kwa kosa la kwenda mahakamani.  Wambura amesema kitendo alichofanya Rais wa Simba Evans Aveva cha kuwasimamisha wanachama hao ni kuchochea migogoro.
Wambura akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam

Wambura alikwenda mbali zaidi kwa kusema hana haja ya kujadiliwa kwenye mkutano wa Agosti 3, kwa kuwa alishasafishwa kwenye Kamati ya rufaa ya uchaguzi iliyochini ya Mwenyekiti wake Julius Lugaziya. 
“Mimi nilishasafishwa kwenye kamati ya Lugaziya na ndio mana nilirudishwa kwenye uchaguzi, na niliondolewa kwa kosa la kufanya kampeni tu hivyo sina haja na mkutano wao,”alisema 
 
Alisema kwa mujibu wa Katiba ya Simba ibara ya 41(d) kuwanyima wanachama fursa ya kujitetea na kusikilizwa kabda ya hatua ni uvunjifu wa haki za msingi za binadamu. Kama zinavyoanishwa kwenye katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13(6)a pamoja na kanuni za nidhamu za FIFA ibara ya 94(1) na kanuni za adhabu za TFF Ibara ya 35 (1). 
 
Wambura ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa TFF alisema wanachama waliokwenda mahakamani wana hoja za msingi hivyo wasipuuzwe. 
“Wangekuwa hawana hoja hata mahakama kuu isingewapa haki ya kufungua shauri lao, hivyo wasipuuzwe wapewe nafasi ya kusikilizwa,”alisema.  Wambura ambaye hii ni mara ya tano kuenguliwa kwenye uchaguzi alisema kitendo alichofanya Aveva ni cha kidikteta  na kitasababisha kuanzisha mtafarakano upya ndani ya klabu hiyo. 
 
Alisema kwa mujibu wa katiba ya Simba Ibara ya 54 (3), uamuzi wowote wa kufukuza wanachama lazima upigiwe kura za siri na wajumbe theluthi mbili waunge mkono, hili japo sio rahisi kama wanavyorifikiria. 
“Kuna wakati Hassani Dalali alitaka kumpindua Mwina Kadugunda ila baadae alikwama baada ya wanachama kukataa pendekezo hilo,”alisema. 
 
Alisema uongozi wa Aveva hauwezi kupambana na wanachama zaidi ya 500, hawataweza vita hivi na lazima waingie kwenye migogoro. 
Wambura aliishauri uongozi huo utafute suluhisho la mgogoro huo mapema kabda ya mgogoro huo haujawa mkubwa. 
 
Alisema japokuwa hawapewa barua rasmi na Rais wa Simba ila ushauri wake kama wanachama atauwasilisha kwa maandishi kwenye uongozi huo. 
“Haya yote nilioongea leo nitayawasilisha kwenye uongozi wa Simba ili wawe na kumbukumbu kama nimeyaongea,”alisema.
 
credit: Bin zubeiry
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top