Mvunja rekodi: Miroslav Klose ni mfungaji bora katika historia ya kombe la dunia.
Miroslav
Klose amevunja rekodi ya Ronaldo na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi
zaidi katika historia ya fainali za kombe la dunia.
Mshambuliaji
huyo wa Ujerumani alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 7-1
dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia na
kufikisha mabao 16.
Lilikuwa
bao lake la pili katika mashindano baada ya kufunga bao akitokea benchi
katika mchezo dhidi ya Ghana, hatua ya makundi na kumfanya alingane
mabao na gwiji wa Brazil.
Historia: Shuti lililomfanya ashikilie rekodi ya dunia
Miroslav Klose 16 goals
Ronaldo 15
Gerd Muller 14
Just Fontaine 13
Pele 12
Jurgen Klinsmann 11
Gary Lineker 10
Klose
alicheza kwa mara ya kwanza fainali za kombe la dunia mwaka 2002 na
kufunga mabao matatu `hat-trick` katika ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya
Saudi Arabia.
Alifunga
tena bao katika mechi iliyofuata ya makundi ambayo Ujerumani ilitoka
sare ya 1-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, kabla ya kufunga bao la pili
katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Cameroon.
Licha
ya Ujerumani kufika fainali mwaka ule, Klose alishindwa kufunga tena
katika mashindano, akimaliza michuano kwa idadi sawa ya mabao na
Rivaldo, nyuma ya mfungaji bora, Ronaldo aliyefunga mabao 8.
Miaka
minne baadaye, Ujerumani walikuwa wenyeji wa fainali za dunia (2006),
mshambuliaji huyo alifunga mabao matano tena ambayo yalitosha kumpatia
kiatu cha dhahabu.
Alifunga
mabao mawili katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Costa Rica ambao
walishinda mabao 4-2, alifunga mengine mawili katika mchezo wao wa
mwisho wa makundi dhidi ya Ecuador.
Klose
bao lake la mwisho katika fainali za kombe la dunia mwaka huu lilikuwa
katika dakika ya 80. Bao la kusawazisha dhidi ya Argentina kwenye mchezo
wa robo fainali na kufanya matokeo yawe 1-1, na Ujerumani wakashinda
kwa mikwaju ya penati.
Na
mwaka 2010, alifanikiwa kufunga mabao mengine manne: moja kwenye mchezo
wa ufunguzi dhidi ya Australia, lingine katika ushindi wa mabao 4-1
dhidi ya England hatua ya makundi na mawili katika ushindi mnono wa
mabao 4-0 dhidi ya Argentina hatua ya robo fainali.
Post a Comment