Mgeni
rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akiwaonesha wajumbe
wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mfumo wa
Kushughulikia Malalamiko ulioandaliwa na Ofisi hiyo mara baada ya
kuuzindua leo katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo mkoani Tanga.
Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab na
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akiwaonesha wajumbe
wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkataba wa
Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Ofisi hiyo mara baada ya kuuzindua leo
katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo mkoani Tanga. Katikati ni
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab na kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akimkabidhi mgeni
rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) Mkataba wa Huduma kwa
Mteja katika kikao cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo
kilichofanyika leo mkoani Tanga. Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali,
Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab.
Mgeni
rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akimkabidhi cheti
kama zawadi ya Mfanyakazi bora Bi. Sylivia Meku ambaye ni Mtakwimu Mkuu
na Mwenyekiti mpya wa TUGHE –Tawi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika
kikao cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika
leo mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA NBS, TANGA)
Post a Comment