Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchmbi (wa nne kutoka kushoto) akiwaongoza
wadau waliofika kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa
barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha
lami kuomba Dua ili mradi huo ukamilike kwa wakati bila kukwamishwa na
changamoto mbalimbali. Sherehe hizo zilifanyika mapema Julai Mosi, 2014
kijijini Kolo Wilayani Kondoa.
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe
alioambatana nao wakikagua magari yanayotumika kwenye ujenzi wa barabara
ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami Mapema
jana wakati wa maadhimisho ya kusherehekea kuanza kwa ujenzi wa mradi
huo yaliyofanyika Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa, wengine pichani ni
wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga
barabara hiyo kipande cha Bonga-Mela (88.8KM).
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi Dereva Abuu Ally Funguo
ya kuwashia mitambo ya kujengea barabara kuashiria kuanza rasmi kwa
Ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa
kiwango cha lami wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa
mradi huo zilizofanyika mapema Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo Wilayani
Kondoa, Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini Mhe. Zabein
Mhita.
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (Katikati mwenye kilemba) na ujumbe
alioambatana nao wakipatiwa maelezo ya mradi wa barabara kutoka Mayamaya
Dodoma hadi Bonga Babati kutoka kwa wakandarasi wa Kampuni inayojenga
barabara hiyo ya China Railway Seventh Group wakati alipotembelea kambi
ya kampuni hiyo iliyopo kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa mapema Julai
Mosi, 2014
Wakandarasi
wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka
Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) kwa
kiwango cha lami wakisikiliza salamu ya Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo
pichani) wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo
zilizofanyika Julai Mosi, 2014 kwenye Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa.
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, wadau, Mafundi na Wataalamu wa Kampuni ya China Railway
Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga
Babati kwa kiwango cha lami kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) wakiwa
kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za
kuanza kwa ujenzi wa mradi huo wa barabara zilizofanyika Kijijini Kolo
Wilayani Kondoa Mapema Julai Mosi, 2014.
Sehemu ya
Wananchi wa Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa waliojitokeza kwa wingi
kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya kutoka
Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami wakisikiliza
salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani), Sherehe hizo zilifanyika
mapema Julai Mosi, 2014. Picha na John Banda wa Pamoja Blog
Post a Comment