Dr. Leonard Maboko Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ya TAG ambae pia ni Mkurugenzi wa NIMR, akitoa neno kwa wageni
Na James Festo, Njombe.
MKUU wa Mkoa wa Njombe Capten Mstaafu Assery Msangi, amezitaka taasisi mbalimbali za kijamii na za kidini Nchini kuendelea kusiadia serikali katika kutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi ikiwemo sekta ya afya.
Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa vyandarua 3100 vinavyotarajiwa kusambazwa kwenye hospitali 11 pamoja na vituo vya Afya 25 vilivyopo katika Mkoa wa Njombe kutoka kanisa la Tanzania Assemblies of God ambalo linaendelea kutoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya jubilii ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwake.
Wakati huo huo Msangi aliwataka viongozi wa kidini nchini kuendelea kuliombea taifa katika msimu huu wa mchakato wa kuipata katiba mpya , sambamba na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni pamoja na uchaguzi mkuu wa mwakani.
Kwa upande wake askofu wa kanisa la T. A. G Njombe, Patrick Saimon Luhwango akisoma taarifa ya ugawaji wa vyandarua hivyo alisema kuwa mkoa wa Njombe umepewa vyandarua hiyvo kwa lengo la kuwakinga na ugonjwa wa maralia.
Alisema kuwa idadi ya vyandarua ambavyo vimegawiwa kwa mikoa mitatu ya Njombe, Rukwa Mbeya inatokana na upembuzi yakinifu uliofanywa na wataalamu kutoka kanisa hilo kwa kushirikiana na waganga wa hospitali za wilaya za mikoa hiyo ambapo uliobaini kuwepo kwa uchache wa vyandarua hivyo.
Thomas Lujuo ni kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe alikiri kuwepo kwa uchache wa vitendea kazi pamoja na vyandarua katika hospitali zilizopo mkoani hapa hivyo vyandarua vitasaidia kupunguza wagonjwa wapya, ambapo marelia kwa mwaka jana ili kuwa na asilimia 11 ya magongwa.
" Msaada huu wa vyandarua ambao tumeupata ni muhimu sana kwa sababu kuna maeneo yana idadi kubwa ya wagonjwa wa maralia hususani katika wilaya ya Ludewa kwa hiyo kupata masaada huu utatusaidia sana sisi kama mkoa kupunguza vifo vitokanavyo na maralia hasa kwa mama wajawazito" alisema Mganga huyo.
Katika hatua nyingine Kaimu mganga huyo alibainisha kuwepo kwa tatizo la utumiaji wa vyandarua kwa wananchi hivyo kuongeza idadi ya wagonjwa maralia licha ya kuwepo kwa utoaji wa vyandarua bila malipo kupitia mpango wa kudhibiti marelia kwa akina mama wajawazito.
Awali akisoma taarifa hiyo mbele ya viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe Askofu Luhwago alisema kuwa katika jubilii hiyo wanatarajia kugawa vyandarua 8550 kwenye hospitali 34 pamoja na vituo vya afya 83 kutoka mikoa hiyo mitatu na kubainisha kuwa wanatarajia kuhitimisha jubilii hiyo julai 13 mwaka huu jijini mbeya katika uwanja wa sokoine ikiwa na kauli mbiu isemayo kuwa" Mungu anajali roho yako na mwili wako, jenga mahusiano naye" huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Raisi wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania.
Post a Comment