Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MLINZI WA SHAMBA ADAIWA KUJINYONGA KWENYE CHUMBA ANACHOLALA

 

MKAZI wa Mbezi Msakuzi, Dar es Salaam, Hassan Ngoso (48), ambaye ni mlinzi wa Shamba, amefariki dunia baada ya kujinyonga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 10 jioni.
Alisema Ngoso alikutwa amejinyonga huku mwili wake ukiwa unaning’inia kwenye kamba aliyofunga katika chumba alichokuwa analala.
Kamanda Wambura alisema nyumba hiyo ipo katika shamba linalomilikiwa na tajiri yake aitwaye Sinyakos Mombeki (45). Sababu za kujinyonga bado hazijafahamika, na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Tumbi.
Katika tukio jingine, mwanamke anayekadiriwa  kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari alipokuwa anavuka barabara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema ajali hiyo ilitokea juzi, saa 8 mchana barabara ya Kilwa, eneo la Kizuiani na kuhusisha gari T 158 AGD aina ya Scania lenye tela T 198 BMZ. Dereva wa gari hilo alikimbia baada ya ajali hiyo.
Wakati huo huo, baadhi ya mabanda ya kuhifadhia nguo katika soko la Ilala, Dar es Salaam, yameteketea kwa moto uliozuka juzi, saa 5 usiku.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top