Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTOTO AOKOTWA GETINI

MTOTO mwenye umri unaokadiriwa kuwa mwaka mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, aliokotwa huko Kibamba CCM, jijini Dar es Salaam, nje ya geti la nyumba ya Getruda Gervans.
Mtoto aliyetelekezwa (jina halikufahamika), mwenye umri unaokadiriwa kuwa mwaka mmoja.
Tukio hilo lilitokea  Juni 24, mwaka huu saa moja na nusu asubuhi huku mfuko wenye nguo zake ukiwa pembeni yake.
Mtoto huyo akiwa amebebwa na msamaria mwema.
Kwa mujibu wa mama mwenye nyumba hiyo, baada ya kumuokota, alimpeleka Kituo cha Polisi Mbezi ambako nako walimpeleka katika Hospitali ya Mwananyamala kabla ya kuhamishiwa Muhimbili.

Afisa ustawi wa  Jamii wodi  ya  watoto Muhimbili, Grace  Julius alilithibitishia gazeti hili kumpokea mtoto  huyo Juni 25, mwaka huu akitokea Hospitali ya Mwananyamala na akatumia fursa hiyo kulaani tabia ya kutupa watoto.
Mifuko na baadhi ya nguo zilizookotwa zikiwa pamoja na mtoto huyo.
Aidha, aliomba mtu  yeyote  mwenye taarifa ya kupotea kwa mtoto sehemu yoyote kufika katika Hospitali  ya Taifa  Muhimbili ambapo alisema kwa taarifa zaidi apige simu namba 0788366399.
Mtoto huyo akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mhariri: Tunakemea vikali vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi  ya watoto na tunawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa mamlaka zinazohusika endapo watamuona mtu yeyote akiwanyanyasa au kuwafanyia ukatili wowote watoto.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top