Afisa
Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha
Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, (kulia)
akisalimiana na Mtendaji wa Kata ya Mnyuzi, Bw. Gosbert Ishengoma mara
baada ya kuwasili kwenye ofisi za kata hiyo wilayani Korogwe. Katikati
ni Afisa Usafi na Mazingira wa Wilaya ya Korogwe, Bw. Frederick Linga.
********************************
Na Mwandishi wetu, Korogwe
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limezindua
mradi wa mamilioni katika eneo la hifadhi Usambara Mashariki, kwa
mafunzo kwa wakazi waliomo na wanaozunguka hifadhi ya Usambara
Mashariki.
Mradi
huo ambao umelenga kuwainua wanavijiji kiuchumi huku wakitunza
mazingira umepata fedha kutoka Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la
Kimataifa la Korea ( KOICA).
Mradi
huo unaotekelezwa katika vijiji 19 vinavyozunguka Hifadhi Hai ya
usambara mashariki ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uchumi wa kijani
ndani ya hifadhi hai(GEBR).
Mradi
huo utawawezesha wananchi kwenye vijiji hivyo kutumia raslimali zao kwa
namna endelevu. Mradi huo unaojulikana kama “Green Economy in
Biosphere Reserves (GEBR)”,wenye thamani ya shilingi milioni 700
utapunguza ukataji miti na kulinda hifadhi kwa kutumia raslimali kwa
busara zaidi.
Mradi
huo unatarajiwa kuwezesha wananchi wa maeneo hayo kupunguza umaskini
kwa kutumia raslimali zilizopo kwa busara na wakati huo huo kuhifadhi
mazingira.
Afisa
Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha
Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, akisaini
kitabu cha wageni kwenye ofisi za kata ya Mnyuzi mara baada ya kuwasili
wilayani hapo kwa ajili ya kuzindua mradi wa mamilioni katika eneo la
hifadhi Usambara Mashariki, na kuendesha mafunzo kwa wakazi waliomo na
wanaozunguka hifadhi ya Usambara Mashariki.
******************************
Baadhi
ya shughuli zitakazofanyika katika mradi huo ni mafunzo ya kuwawezesha
wananchi kufanya shughuli za kiuchumi katika hifadhi ambayo
yalifunguliwa leo na Mjumbe wa Kamati ya Hifadhi Hai Tanzania, Joseph
Kigula.
Mafunzo
hayo kwa vijiji vitatu ambayo yanaendeshwa na EUBR na Wizara ya Mali
Asili na Utalii wanavijiji watafunzwa masuala ya menejimenti ya
biashara, soko, uhasibu, fedha, ujasiriamali mazingira na elimu ya
hifadhi.
Elimu
hiyo inatarajiwa kupanua uelewa wanakijiji kuhusu mahusiano ya biashara
na hifadhi ya mazingira na kujenga uwezo wa ujasairiamali.
Mafunzo mengine mawili yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka.
Mmoja
wa wajasirimali, Jason J Drew alisema kwamba mazingira yamekuwa
yakiathirika sana katika shughuli za kiuchumi na watu kuachana na dhana
ya hamsini kwa hamsini.
UNESCO
imesema ni matumaini yake kwamba katika mradi huu, mazingira ya maeneo
hayo yataendelea kuneemeka huku wananchi wakifanya shughuli za kiuchumi.
Baadhi
ya wanakijiji wa kata ya Mnyuzi wakitoa burudani kabla ya ufunguzi
rasmi wa mafunzo hayo yaliyoanza jana kwenye hoteli ya SB Palace kata ya
Mnyuzi wilayani Korogwe.
***********************************************
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa mradi huo, Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hifadhi
Hai Tanzania, Bw. Joseph Kibula alisema kuwa mradi huo ambao
unatekelezwa katika maeneo ya Usambara Mashariki hapa nchini utawezesha
wananchi wanaoishi kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi kutunza
mazingira lakini kujiendeleza kiuchumi.
Kibula
alisema nia kubwa ya mradi ni kukuza uchumi wa wananchi kwa kupitia
njia zilizoboreshwa ambazo haziathiri rasilimali za misitu sambamba na
kuanzisha biashara za kijani kwa ajili maendeleo endelevu ya wakazi wa
maeneo hayo.
“Matarajio
ni kuzijengea uwezo jamii za vijiji zenye bidhii ya kuhifadhi bioanuwai
na kupunguza athari dhidi ya rasilimali za misitu …ili ziweze kutafuta
riziki kwa maendeleo endelevu”,alisema Kibula.
Kwa upande wake, Afisa Mradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko,
alisema wanatarajia elimu hiyo ilete mabadiliko chanya kwa wananchi
kaika kupunguza umaskini na kufanya biashara za kijani kwa maendeleo
endelevu ya jamii wa Hifadhi Hai ya Usambara Mashariki.
Ko
alisema kuwa kutokana na ushahidi wa huduma zitokanazo na
bioanuwai,biashara ya kijani ni zana itakayowezesha kuhifadhi na kuleta
maendeleo endelevu kupitia mgawanyo wa maslahi unaolingana.
Afisa
Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha
Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko akijumuika na
baadhi ya wanakijiji wa Mnyuzi kucheza ngoma ya asili aina ya Mdumange
kabla ya kufungua mafunzo hayo.
***************************
“Mradi huu unatoa fursa kwa jamii zilizopo na zilizopakana na hifadhi
hai nchini Tanzania katika njia ya mazingira rafiki na uchumi wenye
neema hususan Hifadhi Hai ya Usambara Mashariki…tunaamini kwa kupitia
mradi huu na elimu hii mtaweza kujipatia utajiri mkubwa kwa kupitia
shughuli za kiuchumi mtakazozifanya”,alisisitiza Mwakilishi huyo wa
Unesco na Koica.
Nao
baadhi ya wananchi waliopewa elimu hiyo walishukuru na kusema kuwa
itawasaidia kupata mbinu za kufanya shughuli za kiuchumi kwa kutumia
rasilimali zinazowazunguka.
“Katika
utunzaji na uhifadhi wa mazingira tunafanya shughuli mbalimbali ikiwemo
ufugaji wa nyuki,vipepeo na hata shughuli za mikono kwa akina mama
hivyo elimu hii ya ujasiriamali itatuwezesha sana kujiinua kiuchumi na
kuondokana na umaskini”,alisema Ayubu Rashid mkazi wa Kijiji cha Mnyuzi.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Mambo ya Kale Taifa, Bw. John Kimaro ( wa pili kushoto)
akifurahi jambo na Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai
(GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung
Su Ko (kushoto) wakati wa burudani huku mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati ya
Kitaifa ya Hifadhi Hai Tanzania,Bw. Joseph Kigula (wa tatu kushoto)
akingalia taswira mbalimbali alizochukua kupitia "Tablet" yake.
*************************************
Kwa
mujibu wa UNESCO asilimia 38 ya ardhi ya tanzania imekaliwa na misitu
ambayo ni muhimu kayika maisha ya wanadamu na viumbe hai.
Hata hivyo inaaminika kwamba asilimia 75 ya watanzania wanaishi vijijini wakitegemea zaidi maliasili na kilimo.
Wamesema
utegemezi huo umekuwa kikwazo kikubwa katika hifadi ya misitu ambayo
imekuwa ikivamiwa kwa ajili ya mahitaji ya nishati na mbao.
Mradi wa GEBR unagusa wilaya ya Muheza, Mkinga, na Korogwe .
Mkuu
wa msafara wa ugeni huo Mhifadhi Hifadhi ya Mazingira asili Amani, Bi.
Mwanaidi Kijazi akitoa utambulisho wa meza kuu kwa washiriki wa mafunzo
hayo kutoka vijiji 19 (hawapo pichani) watakaonufaika na mradi huo.
Mgeni
rasmi Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hifadhi Hai Tanzania, Bw. Joseph
Kigula, akizungumza wakati akizindua rasmi mafunzo kwa washiriki kutoka
vijiji 19 vinavyozunguka Hifadhi Hai ya usambara mashariki ikiwa ni
utekelezaji wa mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai(GEBR)
unaoratibiwa na UNESCO kwa ufadhili wa KOICA. Kulia ni Mwenyekiti wa
Kata ya Mnyuzi, Bw. Juma Mkunguti, Kutoka Kushoto ni Afisa Mradi wa
Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko,
Mhifadhi Hifadhi ya Mazingira asili Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi na
Mkurugenzi Msaidizi wa Mambo ya Kale Taifa, Bw. John Kimaro.
Afisa
Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha
Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (wa pili
kushoto) akizungumza na washiriki na kuelezea lengo la mradi huo ambapo
amesema unalenga kuwakomboa kiuchumi na kupunguza umaskini kwenye jamii
zao. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa msafara wa ugeni huo Mhifadhi Hifadhi ya
Mazingira asili Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi akitafsiri kwa washiriki.
Mkufunzi
wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara
yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw. Mussa
Mashishanga akitoa mada ya namna ya kutafuta masoko kwenye mafunzo ya
kuzijengea uwezo jamii za vijiji zenye bidii ya kuhifadhi bioanuwai na
kupunguza athari dhidi ya rasilimali za misitu ili ziweze kutafuta
riziki kwa maendeleo endelevu yanayofanyika kwenye Hoteli ya BS Palace
kata Mnyuzi wilayani Korogwe.
Pichani
juu na chini ni Sehemu ya washiriki kutoka vijiji 19 vinavyozunguka
Hifadhi Hai ya Usambara mashariki ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa
uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai(GEBR) wakifuatilia kwa umakini
mafunzo hayo.
Mshauri
na Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha
biashara yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw.
Lawrence Ambokile akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa mafunzo hayo.
Mgeni
rasmi Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hifadhi Hai Tanzania Joseph Kigula
(walioketi wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi
pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
Post a Comment