MTOTO Omari Hamduni (3) mkazi wa Keko Magurumbasi jijini Dar es
Salaam, amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo alisema kifo hicho
kilitokea jana saa 5 asubuhi jirani na eneo alilokuwa akicheza mtoto
huyo.
Alisema mama wa mtoto huyo alikuwa akifanya shughuli nyingine za
nyumbani ndipo ghafla aliposikia kelele za watu waliomuona Omari
akitumbukia kisimani.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, mtoto huyo aliokolewa, lakini alifia njiani akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke.
Post a Comment