****
Agnes Marwa
(18 ) mkazi wa kijiji cha Mrito,Tarime Mara amesema kutokana na ukatili
aliofanyiwa na mumewe hayuko tayari kurudi kwa mwanamme huyo ingawa ni
mwaka mmoja sasa tangu waoane na kuwa na ujauzito wa mwezi mmoja na
nusu.
Marwa Chacha anatuhumiwa kumpiga,kumfunga kamba na kumweka nje wakati
mvua inanyesha ,kisha akaenda jikoni na kuchukua kijinga cha moto na
kuanza kumuunguza sehemu zake za siri baada ya kukuta shilingi 2000
kwenye pochi yake na kumtuhumu kuwa amepewa fedha hizo na wanaume julai
13 mwaka huu.
Baada ya
kitendo hicho mtuhumiwa alitoroka na Agnes kwa mila za kikurya alificha
tukio hilo hadi julai 17 mwaka huu ndipo akapelekwa katika kituo cha
afya cha Sungusungu kilichopo Nyamongo.
Mganga
mfawidhi wa kituo cha afya Sungusungu Kagumilwa Kaijage amesema kuwa
siku aliyofikishwa kituoni hapo alikuwa na hali mbaya kwani alikuwa
akitokwa usaa katika sehemu zake za na mapajani kutokana na kuunguzwa
sehemu hizo.
Jeshi la
Polisi kanda maalum ya Rorya limesema mtuhumiwa pamoja na mama yake
wametoroka na hii ni baada ya kutoa taarifa,hata hivyo jeshi hilo bado
linaendelea kufanya utafiti ili liweze kumkamata mtuhumiwa.
Post a Comment