Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika
Godfrey Zambi (pichani) ametoa siku mbili kwa bodi ya pamba Tanzania kanda ya magharibi
kuhakikisha inalimaliza mara moja tatizo la wakurugenzi wa halmashauri za
wilaya katika mkoa wa Simiyu la kuyatoza ushuru makampuni ya kununua pamba
ambao tayari unalipwa na serikali.
Agizo hilo amelitoa jana wakati wa
majumuisho ya ziara yake ya siku mbili wilayani Kahama baada ya kuelezwa kuwa
makampuni ya kununua pamba katika mikoa ya shinyanga na simiyu Mkoani Simiyu yamepata
pingamizi kubwa la kutozwa ushuru ambao tayari serikali imeufuta.
Kabla ya hapo taarifa ya makampuni hayo
ya kununua pamba katika mikoa hiyo iliyotolewa na meneja wa Kampuni ya Kahama
Oil Mill ya mjini Kahama Wiliam Matonange imeeleza kuwa mkoani Simiyu
halmashauri zote zimezuia pamba isinunuliwe bila kulipa Ushuru huo
Hali hiyo imemshangaza waziri Zambi
ambaye amesema serikali tayari imetenga shilingi bilioni 10 kwa ajili ya
kufidia shilingi 30 kwa kila kilo itakayonunuliwa fedha ambayo zitalipwa
halmashauri zote zenye zao la pamba kwa
lengo la kufidia ushuru huo
Zambi alisema serikali iliona itoe fedha
hiyo ili iyafanye makampuni yanunue zao hilo kwa shilingi 750 kwa kilo badala
ya 720 kwa kilo kama yangeendelea kulipa ushuru huo katika halmashauri hizo.
Kufuatia hali hiyo waziri zambi
alimuagiza mkurugenzi huyo wa bodi ya pamba Tanzania kanda ya magharibi Buluma
Kalidushi kulimaliza tatizo hilo baada ya hapo atalifikisha kwa waziri mkuu
aliyetoa agizo hilo la kufuta ushuru huo katika halmashauri za wilaya zenye zao
la pamba
Post a Comment