Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
Asifiwe George na Victoria Kanje (RCT), Dar es Salaam
JESHI la
Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam limeanza uchunguzi kuhusu kifo cha
Balozi wa Libya nchini, Ismail Hussein Nwairat (39) ambaye alijipiga
risasi juzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, alisema balozi
huyo alifariki Julai mosi, mwaka huu saa 13:15 mchana kwa kujipiga
risasi.(Martha Magessa)
Balozi Nwairat alijiua kwa kujipiga risasi akiwa amejifungia ndani ya Ofisi ya Ubalozi wa Libya, uliopo Mtaa wa Mtitu, Upanga.
Kova
alisema hivi sasa Jeshi hilo linafanya uchunguzi, ikiwamo kujua sababu
za Balozi huyo kuamua kujiua na tayari wamepatiwa kibali cha kuanza kazi
hiyo.
"Uchunguzi
huo utawahusisha wataalamu wa kuchunguza vifo vya aina hii kutoka Jeshi
la Polisi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Libya na Wizara ya Mambo ya
Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ili kukamilisha uchunguzi huo
pamoja na hatua nyingine muhimu za tukio hili," alisema Kova.
Kaimu
Balozi Nwairat amejiua kwa kujipiga risasi ofisini kwake juzi, hadi sasa
bado haijafahamika ni kwanini amechukua uamuzi huo.
Balozi Nwairat alijifungia ofisini kwake na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.
Wakati
huo huo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza linafanya
uchunguzi kuhusu tukio la kushambaliwa kwa basi la Magereza namba T0046
aina ya Isuzu, lililotokea juzi Mikocheni, jijini Dar es Salaam, jirani
na Regency Hotel.
Kova
alisema tukio hilo lilitokea saa 13:30 mchana ambapo watu wasiofahamika
walilishambulia basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Askari Magereza
namba A.9716 SGT Msofe.
CHANZO:MTANZANIA
Post a Comment