Kulia Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkamia akipeana mkono na Meneja Mkuu wa
Kampuni ya Bakhresa Group Said Muhammad Said Abeid mara baada ya kumkabithi
Hundi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 93,000 kutoka kwa Kampuni ya Bakhresa
Group kwa ajili ya kusaidi timu za wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya
Jumuiya ya Madola jijini Glasgow Scotland.Makabidhiano hayo yamefanyika katika
Ukumbi wa Wizara ya Habari leo jijini
Dar es Salaam .
Kutoka kulia Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkami,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Meneja Chapa
wa Kampuni ya Bakhresa Group, Katibu wa Naibu Waziri Bw. Francis Songoro na
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Bw.Said Muhammad Said Abeid wakifurahia mara
baada ya makabidhiano ya hudi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 93,000/= ikiwa
ni msaada wa kampuni hiyo kwa wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya
Madola nchini Scotland.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Juma Suleiman Nkamia akizunguza na waandishi wa habari wakati wa
hafla ya kupokea msaada wa Hundi yenye thamani ya Dollar za Kimarekani 93,000
kutoka kwa Kampuni ya Bakhresa Group kwa ajili ya kusaidi timu za wanamichezo
wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola jijini Glasgow Scotland jijini Dar
es Salaam leo, katikiti ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Said Muhammad
Said Abeid na Meneja Chapa wa Kampuni hiyo Bw. Abubaker S.A.
Baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia
makabidhiano ya hundi ya mfano kutoka kwa wawakilishi wa Bakhresa Group katika
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo leo jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo imetoa msaada wa Dola za
Kimarekani 93,000 ili kusaidia timu za wanamichezo wanaoshiriki Mashindano ya
Jumuiya ya Madola yanayotaraji kuanza rasmi tarehe 23 mwezi huu huko mjini
Glasgow Scotland.
Picha na Frank Shija
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini., WHVUM
Post a Comment