Timu
ya taifa ya soka ya Ujerumani imewasili nchini humo kwa kishindo wakiwa
na kombe lao la ushindi walilolinyakua katika mashindano ya kombe la
dunia ambyo yalikamilika juzi nchini Brazil.
Maelfu ya mashabiki wa soka wamekuwa wakisubiri tangu asubuhi na mapema mjini Berlin kuwakaribisha wachezaji hao.
Sherehe
zitafanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambako wachezaji
wataonyeshea kombe lao, ambalo walilishinda katika fainali ya mashindano
hayo dhidi ya Argentina.
Shangwe na vigelegele vimeshuhudiwa huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kushuhudia kombe hilo ambalo litapitishwa mjini kote.
Watu wengi wamenunua jesi zenye nyota nne kuashiria ushindi wa nne wa nchi hiyo katika kombe la dunia.
Wachezaji wa timu hiyo ambao huchezea timu ya Bayern Munich pia watapata ukaribisho mkubwa baadaye mjni Munich.
Mwandishi
wa BBC Steve Evans ambaye yuko mjini Berlin anasema kuwa watu nusu
milioni wanatarajiwa kukutana na wachezaji hao mjini Berlin.Chanzo BBC
Swahili
Post a Comment