Semina
na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wa
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na baadhi ya wale wa
daraja la kwanza wenye kiwango cha juu (elite) itafanyika jijini Dar es
Salaam.
Waamuzi
30 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watashiriki kwenye semina hiyo
itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Julai 21 hadi 26
mwaka huu.
Mkufunzi
wa FIFA kwa Kanda ya Kusini mwa Afrika, Carlos Henriques kutoka Afrika
Kusini ndiye atakayeendesha semina hiyo akisaidiwa na Watanzania Charles
Mchau kutoka Kilimanjaro, Juma Ali David (Zanzibar), Joan Minja (Dar es
Salaam) na Riziki Majala (Pwani).
Waamuzi
na waamuzi wasaidizi wa FIFA watakaoshiriki semina hiyo ni Ferdinand
Chacha (Mwanza), Hamisi Chang’walu (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar
es Salaam), Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya), Josephat
Bulali (Zanzibar), Kinduli Ali (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam),
Ramadhan Ibada (Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha
(Zanzibar).
Kwa
upande wa waamuzi wa daraja la kwanza ni Abdallah Kambuzi (Shinyanga),
Agnes Pandaleo (Arusha), Ahamada Simba (Kagera), Arnold Bugado
(Singida), Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Frank Komba
(Pwani), Helen Mduma (Dar es Salaam), Issa Bilali (Zanzibar) na Issa
Haji (Zanzibar).
Wengine
ni Janeth Balama (Iringa), Jonesia Rukyaa (Kagera), Lulu Mushi (Dar es
Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mbaraka Haule
(Zanzibar), Mfaume Ally (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga) na Soud Lila
(Dar es Salaam).
Washiriki wa semina hiyo na wakufunzi wanatakiwa kuwasili jijini Dar es Salaam, Julai 20 mwaka huu.
Post a Comment