Julius Mtatiro
SIRI
ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba
kufanya mabadiliko kwenye kurugenzi zake kwa kumng’oa Julius Mtatiro
kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, imefichuka.
Vyanzo
vya habari kutoka ndani ya chama hicho, vinadai kuwa sababu ya kwanza
imetokana na viongozi wakuu wa chama hicho taifa kumtaka Mtatiro
asigombee nafasi yoyote.
Inaelezwa
kwamba Mtatiro aliandaliwa kisaikolojia kwamba hatarudi kwenye nafasi
yake kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji wake.
Sababu
ya pili ambayo inatajwa na baadhi ya viongozi wa CUF ni kwamba kiongozi
huyo kijana, anadaiwa kujihusisha na matumizi mabaya ya fedha hasa
wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga.
Kwa
mujibu wa habari hizo, sababu ya tatu inaelezwa kuwa Mtatiro alikuwa
akifanya siasa za kitoto (siasa nyepesi), zilizokuwa zinawakera baadhi
ya viongozi wa juu wa CUF.
“Mtatiro
sio kama amependa mwenyewe kuacha nafasi hiyo la hasha, ukweli ni
kwamba aliandaliwa kisaikolojia kuwa nafasi hiyo hatoshi na inamlazimu
atoke ampishe Sakaya ambaye anaweza akasukuma gurudumu hilo la chama,”
kilieleza chanzo cha habari hizo.
CUF imefanya mkutano mkuu na kuwachagua wajumbe wapya wa Baraza Kuu pamoja na kurugenzi.
Katika mabadiliko hayo, nafasi ya Mtatiro inachukuliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya.
Nafasi
ya Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, imeshikiliwa na Joran Bashange,
Mkurugenzi wa Haki na Binadamu na Sheria imeshikiliwa na Mbunge wa Viti
Maalumu Rufiji, Rukia Mchuchuli huku nafasi ya Kurugenzi ya Mipango na
Uchaguzi imeenda kwa Shaweji Mketo.
Wapinga mabadiliko
Baada
ya kufanya mabadiliko hayo, baadhi ya wanachama wamejitokeza kupinga
uteuzi huo na leo wanatarajia kufanya maandamano ya amani kwa lengo la
kuonana na kuzungumza na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba kueleza
sababu za kutoridhishwa na baadhi ya viongozi.
Akizungumza
na Tanzania Daima jana, Ibrahimu Nanga, ambaye ni mmoja wa wanachama
wanaopinga uteuzi wa baadhi ya viongozi, alisema watakwenda kuwataka
viongozi kuwapa fursa ya kueleza dukuduku lao.
“Lengo
si maandamano bali ni kutaka kukutaka na mwenyekiti. Tunapinga uteuzi
wa Shaweji Mketo na wengine waliorejeshwa wakati kipindi kilichopita
hawakukisaidia chama,” alisema Nanga.
Tanzania Daima
Post a Comment