Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ray, Johari sasa kugawana hadi nguo za Ndani

 
ray

Hali katika kampuni ya RJ inayoongozwa kwa ubiya kati ya Vicent Kigosi ( Ray) na Blandina Chagula ‘Johari’, inazidi kuwa tete kwa kile kinachoelezwa kuwa johari hataki kufanya kazi pamoja na ‘mke mwenza’ Chuchu Hans.
Chanzo hicho ambacho kipo karibu na wasanii hao kilisema kuwa mwezi mmoja uliopita Johari na Chuchu, walikuwa katika kuelekea kuelewana ambapo johari, alishakubali yaishe kuwa Ray wake ameshapokonywa na mtoto huyo wa Kitanga .
Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa baada ya Johari kuwa katika hali hiyo,ndipo Chuchu alipoanza kutanua makucha yake ndani ya kampuni kwa kujifanya ni mmoja kati ya wakurugenzi wakati ukweli haupo hivyo.
Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa imefikia hatua Chuchu, kaanza kutoa amri kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo bila ya kupata kibali kutoka kwa wakurugenzi waasisi ambao mtaji wao unadaiwa kutokana na Johari ‘kumpiga’ changa la macho mfanyabiashara maarufu kutoka mkoani Mbeya.
 
Mpashaji huyo alizidi kusema kuwa bifu liliibuka upya mkoani Dodoma, ambako Ray na Johari walikwenda katika ziara ya Kilimanjaro Music Awards Tour, na mashabiki wao kuwataka wapande jukwaani kwa pamoja.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top