Jumatatu July 07 kwenye moja ya migahawa iliyopo eneo la Uzunguni
Jijini Arusha,Watu wanane waliripotiwa kujeruhiwa katika mlipuko wa
bomu.
Mkurugenzi wa makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi Kamishina Issaya
Mngulu amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa nane usiku ambapo
watu wasiojulikana walirusha bomu hilo ndani ya mgahawa ujulikanao
kama Vama Traditional Indian Cusino uliopo jirani na viwanja vya Gymkhana
jijini Arusha.
Pamoja na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Jeshi la Polisi za
kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na usalama na yenye tulivu,bado
kumeendelea kuwa na matukio ya kiuhalifu yakiwemo ya milipuko katika
maeneo mbalimbali.
Mkurugenzi wa makosa ya jinai anasema>>“Kufuatia kutokea kwa
matukio haya bado tunaendelea na upelelezi wa kina ili kuhakikisha
kwamba wale wote walioko kwenye mtandao huo wanakamatwa na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria’
‘katika tukio hilo la jana tayari watu wawili wanashikiliwa kwa
uchunguzi zaidi lakini pia kati ya wale wanane mmoja wao hali yake siyo
nzuri hivyo amepelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi’.
Pia ameongeza kwa kusema katika matukio mengine ya nyuma yaliyowahi
kutokea mpaka sasa jumla ya watu 20 wamekamatwa wakiwemo sita
wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea Julai 3 mwaka huu
nyumbani kwa Shekhe Ally Sudi mkoani Arusha na wengine 12 katika tukio
lililotokea Zanzibar.
Hata hivyo Kamishina Mngulu ametoa wito kwa wananchi kuchukua
tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, vilevile wawe
makini na mtu ama kitu watakachokitilia shaka.
Post a Comment