ULINZI na usalama watakaowekewa
magwiji wa Real Madrid, maarufu kama `Real Madrid Legends` mara
watakapowasili jijini Dar es salaam, utakuwa wa hali ya juu na serikali
imeahidi kufanikisha hilo kwa asilimia 100.
Nyota waliotikisa soka la dunia
wakiwa na Real Madrid na kushinda mataji ya La Liga, UEFA na wengine
kushinda kombe la dunia na nchi zao watatua nchini Agosti 22 na kucheza
mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa Tanzania, Agosti
23 uwanja wa Taifa.
Kwa mara ya kwanza barani Afrika
Magwiji wa Real Madrid kama vile Luis Madeil Figo, Zinadine Zidane,
Fabio Cannavaro, Ronaldo De Lima, Roberto Carlos, Michael Owen watazuru
Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,
Saidy Mecky Sadick jana ofsini kwake maeneo ya Ilala jijini Dar,
alikutana na kamati ya maandalizi ya ziara hiyo inayoongozwa na
mwenyekiti wake, Farough Baghozah na kuelezwa kila kitu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogpsot.com
Post a Comment