Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Walichoahidiwa Van Persie na wenzie wa timu ya Uholanzi ikiwa watashinda ubingwa wa dunia

Holland
Wakati ikijiwekea rekodi ya ushindi asilimia 100 katika michezo yake yote kwenye kombe la dunia mpaka sasa wakiwa wamefika katika hatua ya robo fainali, timu ya taifa ya Uholanzi ambayo ilikuwa ikipewa nafasi ndogo sana ya japo kuvuka hatua ya makundi, wameahaidiwa zawadi kubwa sana na ya kipekee ikiwa tu wataweka historia ya kutwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya kwanza.

Kampuni ya masuala ya anga ya nchi hiyo iitwayo Ruimtevaartbedrijf SXC aerospace engineering company imeihaidi timu ya taifa ya nchi hiyo safari ya kwenda mwezini ikiwa tu watafanikiwa kubeba ubingwa wa dunia..
Mmoja wa wahasisi wa SXC Michiel Mol alikiambia chombo cha habari cha Uholanzi, NL Times:
“Kama kampuni yenye asili ya kidachi, tunayo furaha kubwa sana na mafanikio ya timu yetu huko Brazil. Kwa kiwango kizuri wanakionyesha basi wanastahili pongezi za aina yake.
“Tutajaribu kuwapeleka wachezaji kwenye kilele cha umbali wa  – 103 km!
“Tutawachukua wachezaji wote 23 na kocha Louis van Gaal.”
 NL Times wanaripoti kwamba, kampuni ya SXC kwa sasa inafanya matangazo ya ndege kwenda mwezini kuanzia mwakani, na kama kila kitu kikienda kama kilivyopangwa na Udachi wakachukua ubingwa wa dunia – basi kikosi kizima cha Udachi kitapata zawadi yao mwaka 2016.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top