TANGAZO
Ubalozi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata
fursa kuja kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda hapo Ubalozini siku ya Jumamosi (tarehe
12 Julai 2014) kuanzia saa nane mchana hadi kumi na moja jioni (14:00 – 17:00
Hours)
Katika Mkutano huo,
Mheshimiwa Pinda anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo ya
nchi yetu. Aidha atajibu maswali kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo.
IMETOLEWA
NA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, LONDON, JUMANNE
(8 JULAI 2014)
Post a Comment