SEHEMU ambayo inasemekana bomu lilitua mara
baada ya kutupwa.
Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo akiongea na waandishi wa habari |
Na Woinde Shizza,Arusha.
Mlipuko
unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo
jijini Arusha katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine
uliopo pembezoni
mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane.
Akithibitisha
kupokea wagonjwa walioathiriwa na bomu
hilo, Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni
kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga
alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya
saa 4:30 usiku katika eneo kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia majira
ya saa tano kasoro na saatano .
Alisema kuwa
walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana
katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna
mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu
kumfanyia upasuaji usiku huo huo.
"kati
yawagonjwa hao nane,mmoja alikutwa akiwa mahututi ,kwani mguu wake ulikuwa umeathiriwa sana na bomu hilo ,ivyo
ikatulazimu kumkata mguu mmoja wa kushoto ,mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa
Deepak Gupta (25) mwanaume,na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupo
katika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani"alisema
Kisanga
Alisema
kuwa katika
majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na
kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya
uangalizi wa madaktari
Aidha aliwataja
majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja
na Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval
(13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush
Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25)
wote wakiwa na asili ya kiasia.
Kisanga alisema
kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio waliofika hapo hospitali
walidai kuwa bomu hilo lilirushwa kwa kupitia
dirishani.
Post a Comment