Referii
muingereza anayefahamika kwa ukakamavu wake Howard Webb ni miongoni mwa
waamuzi 15 walioteuliwa kusalia Brazil kushiriki mechi zilizosalia za
kombe la dunia.
Webb
mwenye umri wa miaka 42 ni miongoni mwa wale watakaotathminiwa kwa uwezo
wao wa kuamua mechi zenye umuhimu mkubwa ikiwemo fainali ya kombe la
dunia huko Brazil.
Webb pamoja na wasaidizi wake Mike Mullarkey na Darren Cann wamekwisha amua mechi mbili za kombe la dunia huko Brazil.
Mpiga kipenga huyo alikuwa muamuzi katika mechi kati ya Colombia na Ivory Coast na pia mechi baina ya wenyeji Brazil na Chile.
Webb
alijiimarisha wasifu wake mwaka wa 2010 alipoamua mechi ya fainali ya
kombe la dunia baina ya uhispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini .
Webb hata hivyo alilaumiwa kwa kukosa kumwadhibu mchezaji Nigel de Jongfor .
Na
baada ya kutizama kanda za video Webb alikiiri kuwa alistahili
kumwonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kadi nyekundu .
Refarii
mmoja pekee kutoka Brazili, Sandro Ricci ndiye aliyesalia kuamua mechi
zilizosalia za nusu fainali fainali na mechi ya kuamua mshindi wa tatu.
Mbali na Brazili Argentina, Ujerumani na Uholanzi ndiyo mataifa yaliyosalia katika kipute hicho.
Refarii kutoka Mexico Marco Rodriguez ndiye atakayeamua mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya Ujerumani na wenyeji Brazil.
Mechi hiyo itachezwa Jumanne .
Rodriguez ndiye refarii ambaye alikosa kumuona mshambulizi wa Uruguay Luiz Suarez akimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.
Post a Comment