ARSENAL
imejiweka katika mazingira mazuri ya kuvuka hatua ya mchujo ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji
Beskitas, Uwanja wa Ataturk.
The
Gunnes walimpoteza nyota wao, Aaron Ramsey aliyeonyeshwa kadi ya pili
ya njano na kuwa nyekundu dakika ya 80 baada ya kucheza rafu.
Mkali
mpya: Demba Ba (kulia) aliyejiunga na Besiktas kwa Pauni Milioni 4.7
kutoka Chelsea msimu huu leo alikuwa mwiba mbele ya mabeki wa Arsenal
Katika
mchezo huo, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba alikaribia
kuifungia Beskitas dakika ya sita baada ya shuti lake kugonga besela,
wakati Alex Oxlade-Chamberlain naye pia alikaribia kuifungia Arsenal
alipogongesha mwamba mwishoni.
Kocha
wa Besiktas, Slaven Bilic pia alipandishwa jukwaani mwishoni mwa
mchezo. Mchezo wa marudiano utafanyika Jumatano ijayo Uwanja Emirates.
Kikosi
cha Besiktas: Tolga, İsmail, Motta, Ersan, Pedro, Olcay/Tore dk72,
Veli, Necip, Ozyakup/Frei dk80, Mustafa/Tosun dk88 na Demba Ba.
Arsenal:
Szczesny, Debuchy, Koscielny, Chambers, Monreal, Arteta/Flamini dk50,
Ramsey, Cazorla/Rosicky dk90, Wilshere, Sanchez/Oxlade-Chamberlain dk72
na Giroud.
Post a Comment