KOCHA
mpya wa Brazil, Carlos Dunga amekibomoa kikosi cha timu hiyo
kilichovurunda Kombe la Dunia kwa kuwatema wachezaji 13 na kuita wengine
wapya.
Philippe
Coutinho ni miongoni mwa ingizo jipya la wachezaji baada ya Kombe la
Dunia baada ya Dunga kuvutiwa na kazi yake akiichezea Liverpool, wakati
Neymar aliyepona majeruhi yake yaliyomfanya akose mechi mbili za mwisho
za Kombe la Dunia ameitwa pia.
Kikois cha wachezaji 22 kimetajwa jana kwa ajili ya mechi mbili za kiradiki dhidi ya Colombia na Ecuador.
Kiwango kizuri: Philippe Coutinho amerejeshwa kikosi cha Brazil baada ya kazi nzuri Liverpool
KIKOSI KIPYA CHA BRAZIL HIKI HAPA...
Makipa: Jefferson (Botafogo), Rafael (Napoli)
Mabeki: Maicon
(AS Roma), Filipe Luis (Chelsea), Alex Sandro (FC Porto), Danilo (FC
Porto), David Luiz (Paris Saint-Germain), Marquinhos (Paris
Saint-Germain), Gil (Corinthians), Miranda (Atletico Madrid)
Voungo: Fernandinho
(Manchester City), Luiz Gustavo (VfL Wolfsburg), Elias (Corinthians),
Ramires (Chelsea), Everton Ribeiro (Cruzeiro), Ricardo Goulart
(Cruzeiro), Oscar (Chelsea), Willian (Chelsea), Philippe Coutinho
(Liverpool)
Washambuliaji: Hulk (Zenit St Petersburg), Neymar (FC Barcelona), Diego Tardelli (Atletico Mineiro)
Post a Comment