Baa iliyopo Sinza-Lion jijini Dar ambayo imegeuzwa kuwa kanisa.
WAKATI matukio mengi ya kushangaza na kushtukiza yakiendelea kutokea kila siku duniani, neno la Mungu nalo linazidi kushika kasi kufuatia baa moja iliyopo Sinza-Lion jijini Dar kugeuzwa kuwa kanisa.Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa baa hiyo maarufu iitwayo The
Don, ukumbi wake ambao ulikuwa ukitumika kwa watu kupiga ulabu, hivi sasa unatumiwa na waumini wa kanisa linalojukana kama Impact International Christian Centre kupata mahubiri. Lakini cha kushangaza ilibainika kwamba katika maandishi makubwa yanayolinadi
jina la baa hiyo, chini yake ndipo limewekwa bango linaloonyesha kanisa
hilo, kitu ambacho kwa mtu mgeni, ni vigumu kuelewa mara moja.
Muonekano wa karibu wa kanisa hilo.
“Siyo baa hiyo kaka, hilo ni kanisa siku hizi, tumeshangaa ghafla tu waumini wanakuja na mhubiri
wao na wanaendelea na sala kama kawaida. Hatujui kama huyu mhubiri
ndiye alikuwa mmiliki wa hii baa au imekuwaje,” alisema jirani mmoja wa
eneo hilo, aliyekataa kutaja jina.
Hata hivyo, juhudi za gazeti hili
kuzungumza na uongozi wa baa au kanisa hilo ziligonga mwamba baada ya
kuambiwa na majirani kuwa ni nadra kuwakuta mahali hapo hivyo jitihada
zinaendelea.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la kuibuka kwa makanisa ya madhehebu mbalimbali, ambayo kila moja huwa na watumishi wao wanaopewa majina kama Mchungaji, Nabii, Askofu na kadhalika.
Post a Comment