![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMyK3bJ_LCTRUIZBd4VWjRfAmHwjVEyh7Op8-iskEn-m4YtoboppRQDBcNbBWqD6eZd6yN4DIvz_NIjHQkBymxuKWpKJzlrwiltzv6dHFljwzp5A7ar3MInsbAolYOuwW4wfd2wexO46JO/s1600/SAM_6495.JPG)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAor4YBfSyF0NLXyn2GDKCHZj85GrCwkBay9rw8VSUXtXV9zYj8lohCnlz82PxHGn6R9BjgKYG3C9zDwRm_W2Y95YhdNAHojmuPSO_6BRNMQ9tEJoCY140ktoavIYuTERTwGYz-mWB-qYR/s1600/SAM_6488.JPG) |
Aliyevaa
nguo ya kijani(CCM) ni bwana Zacharia Mfuko diwani wa CHADEMA kata ya
Masekelo katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwasili katika mkutano
wa Chadema leo jioni,baadaye alivua nguo hizo na kuomba radhi kuwa
alikosea njia baada ya kushawishiwa na viongozi wa CCM akiwemo Stephen
Masele,Nape Nauye, Habib Mchange na viongozi wengine wengi ndani na nje
ya chadema na CCM,na kueleza kuwa ccm hawana lolote badala ya kulaghai
watu. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiZ2s4mrcNmtYQZsmDkmeQk7WdoPg9dyq55IxIxuU0fT1Knm2fRqWuyDPHxEeJfKw_4zWruFFcKbeuE4yXpw7XnB6z8i_ngRLi0HZ_vO1r_pnYPRVaumL7sB8R03b65kqTkZqoncTU6EVR/s1600/SAM_6490.JPG) |
Kulia
ni Sebastian Peter diwani wa Ngokolo akiwasili katika eneo la
mkutano,leo.Katika hali ya kushangaza baada ya madiwani hao kuwasili
kwenye mkutano vurugu za hapa na pale zilitawala takribani dakika 15
lakini baadaye hali ilikuwa shwari baada ya mbunge Kasulumbayi kutoka
jimbo la Maswa mashariki kutumia akili na nguvu nyingi kutuliza
wanachama wa Chadema waliokuwa na hasira na kutopendezwa na kitendo cha
kuwaleta wasaliti wa chama eneo hilo.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbj4nlI1Z3XCiUC0D3uXEcs6l7olASfOdHkQDWp1LoCfrPyJj02HoZlv15Q8FgK5cVSGCI24fAzN-IDZCHTaoTsb-DW-HaAi8ph0mOWQb6X4KMkEmlC7hKQ2xoqR6MaXOvxDxJhUKTlNF4/s640/SAM_6518.JPG) |
Hali ilikuwa tete,ngumi zikanukia,kulia ni mmoja wa viongozi wa chadema
akikabiliana na wanachama wa chadema waliotaka kuleta vurugu uwanjani
hapo.
Madiwani
wasaliti kama wanavyoitwa hivi sasa hapa Shinyanga,wakiwa na nguo za
CCM wakiwa wamekaa na viongozi wa CHADEMA baada ya kuwasili eneo la
mkutano jioni ya leo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_P5S94REZtriP6unRO6XDUq_lDe3FwYOd58lMii0T1gXFtjKVtnask2-Tne5kACKYFdZBmFg2LeV8bDAmdzEztkpuTq1mSyouGqE8LNNTsEekEuwxaqJMEnNMxDrCEhmY9Yxn5x0qJ_tZ/s1600/SAM_6511.JPG)
Mkutano huo ni wa aina yake umehudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga,kila mtu akiwa na lake moyoni.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2QtbEmjWOiz0pn9PIor9fYGKD6mgZcoUFLgzfPEY72cOa_rSP7-tg1sNWozXbVspCVmUX2XOYi-ErD-Mwg2ATziboGz4XS9fUC2NFwbeQPrjaMhUaEyrVDPVZlMKOOmGqui6dzYESSQ9D/s1600/SAM_6506.JPG) |
Diwani Sebastian Peter kulia akinong'ona jambo na mbunge Kasulumbayi.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Hapa ni katika viwaja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa aina yake ambao pengine unaweza kuuita mkutano wa kihistoria,mkutano ambao uliandaliwa na viongozi wa CHADEMA kanda ya ziwa mashariki wakiongozwa na mbunge wa Maswa mashariki Sylivester Kasulumbayi.Katika mkutano huo wale madiwani wa Chadema ambao mwezi Februari mwaka huu,walijiuzulu na kuhamia CCM,Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo na Sebastian Peter kata ya Ngokolo,leo wameomba radhi na kurudi CHADEMA.Miongoni mwa sababu walizozitaja kuchangia kuhama kwao CCM ni chama kinachochonganisha vyama walidanganywa kuhamia ACT lakini wamebaini kuwa ACT na CCM hawana tofauti hivyo kuamua kurudi chadema kwani ndiyo chama imara.Walisema waliahidiwa kuwa wahame Chadema waende CCM ili wajiunge na ACT ili waiimarishe lakini wameshindwa kutofautisha ccm na ACT.Ikumbukwe kuwa walihamia CCM wakidai CHADEMA hakifai kinaendekeza ubinafsi,ukabila n.k,ikafikia hatua wakaitwa madiwani mizigo.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
|
on Friday, August 1, 2014
Post a Comment