Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
IGP Ernest Mangu akisalimiana na masheikh wa mikoa na maimamu wa
misikiti katika ukumbi wa bwalo la maafisa wa Polisi wakati wa kikao
cha muendelezo wa kampeni ya familia yetu haina mhalifu kilichoratibiwa
na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka. Picha na Hassan Mdeme- wa
Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiwa na
Mufti na Sheikh mkuu wa Tanzania Shabani Simba na viongozi wengine wa
dini ya kiislamu wakati wakiingia katika ukumbi wa bwalo la maafisa wa
Polisi kuhudhuria kikao cha muendelezo wa kampeni ya familia yetu
haina mhalifu kilichoratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka.
--
Na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi
Viongozi wa dini wametakiwa
kuendelea kufanya doria za kimwili na kiroho katika kuimarisha ulinzi
na usalama ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwajenga vijana katika
maadili mema na kuacha kutenda dhambi ya kujihusisha na vitendo vya
uhalifu.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu
alipokutana na viongozi wa dini ya kiislam katika ukumbi wa Bwalo la
maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es salaam. Kikao hicho
kiliratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka inayoongozwa na
Sheikh Issa othuman.
Post a Comment