Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTOTO ALIYEKUWA ANASUMBULIWA NA KANSA YA MACHO AFARIKI DUNIA

 

Mtoto Godwin Florence Rweyemamu (3) enzi za uhai wake akiwa na bibi yake, Elda Charles Rweyemamu.
Na Makongoro Oging'
MTOTO Godwin Florence Rweyemamu (3), mkazi wa Kijiji cha Kamala, Kata ya Bangwe mkoani Kigoma aliyeletwa katika Hospitali ya Taifa jijini Dar es Salaam kwa matibabu ya kansa ya macho amefariki dunia leo asubuhi.

Mtoto Godwin amefariki baada ya kusumbuliwa na kansa ya macho iliyoambatana na malaria na upungufu wa damu mwilini.Godwin aliletwa na bibi yake Elda Charles Rweyemamu katika Hospitali ya Muhimbili hivi karibuni wakitokea mkoani Kigoma kwa ajili ya matibabu lakini uchunguzi wa madaktari uligundua kuwa wamemchelewesha hivyo arudishwe nyumbani Kigoma.
Katika harakati za bibi yake kutafuta nauli ya kurudi Kigoma, wananchi walimchangia shilingi milioni 1.2 ikiwa ni pamoja na tiketi ya ndege na walipaswa kuondoka na Ndege ya Shirika la ATC jana Jumamosi saa 11 alfajiri, kabla ya muda huo kufika, saa 9 usiku marehemu alizidiwa kutokana na kuishiwa damu pamoja na malaria ambapo alipelekwa Zahanati ya St. Monica, Manzese kisha Hospitali ya Mwananyama, hali ilipozidi kuwa mbaya alipelekwa Muhimbili.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho Jumatatu katika makaburi ya Mbezi-Makabi jijini Dar.
Bibi wa mtoto huyo ametoa shukrani kwa wale wote waliojaribu kuokoa maisha ya mjukuu wake kwa maombi na michango ya hali na mali.
Kwa yeyote anayependa kuwasiliana na bibi huyo atumie namba  0762 175 1170784 420 215 au 0719 285 100
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top