Kituo
kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa
na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia. Watu kama 20 hadi
30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za ebola walitoroka baada
ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku..
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vyengine. Kituo kiko kwenye
mtaa wa West Point, wenye wakaazi wengi. Mwandishi wa BBC katika kanda
hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa
katika mtaa wao.
Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.
chanzo: bbc
Post a Comment