Mwanawe muigazaji nyota wa Hollywood Jackie Chan amekamatwa kwa madai alitumia mihadarati.
Jaycee
Chan, 31, ambaye mwenyewe ni msanii pamoja na muigizaji kutoka
Taiwanese Kai Ko, 23, walikamatwa alhamisi iliyopita kwa mujibu wa
taarifa ya polisi mjini Beijing .
Polisi
wanasema kuwa wawili hao walipatikana wamevuta bhangi huku mwanawe Chan
akikabiliwa na kosa zaidi la kupatikana na dawa hiyo haramu.
Kukamatwa kwa wawili hao kunawadia wakati polisi wamekuwa wakifanya misako ya dharura na kuwakamata wasanii nyota kadhaa.
Gao
Hu, 40, aliyeigiza katika filamu ya mwaka wa 2011 Zhang Yimou "The
Flowers of War", alikuwa miongoni mwa wasanii wengine wakutajika
waliokamatwa mapema mwezi huu.
HU alipatikana ametumia Bhangi pamoja na madawa aina ya methamphetamines.
Operesheni
hizi zinafuatia agizo la rais wa China Xi Jinping mwezi juni kwa polisi
la kuwataka kuimarisha juhudi za kukabiliana na matumizi ya mihadarati
nchini humo.
Duru
zinaarifu kuwa Kukamatwa kwa mwanawe msanii maarufu zaidi nchini humo
maafisa wa polisi wanajaribu kuwadhibitishia umma kuwa hakuna
atakayeepuka mtego wao .
Mwandishi
wa BBC mjini Beijing Martin Patience anasema kuwa watu wenye sifa kubwa
wanalengwa na maafisa wa polisi kutokana na ushawishi mkubwa walionao
miongoni mwa jamii nchini humo.
Hata
hivyo kiongozi wa idara ya baraza la umma la Beijing inayopambana na
matumizi ya mihadarati bwana Jin Zhihai amekanusha kuwa idara yake
imekuwa ikilenga wasanii na waigizaji nyota katika kampeini yao dhidi ya
matumizi ya mihadarati.
"ikiwa tutaendelea na kampeini hii dhidi ya matumizi ya mihadarati ninahakika waigizaji wengi nyota watakamatwa ''
Juma
lililopita miungano 42 inayowakilisha wasanii walitia sahihi maagano ya
kukataa kuwasajili wasanii waotumia mihadarati katika maonesho yao.
Kampuni inayomwakilisha bwana Chan iliomba msamaha kwa uma kwa niaba yake.
Kampuni hiyo ya M'Stones International iliahidi kumpeleka hospitalini ilikukomesha matumizi ya dawa hizo.
Babake Jackie Chan hajasema lolote kufikia sasa.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment