Wakazi
wa Dar es Salaam ambao ni walemavu wa ngozi (albino) wakionesha hisia
zao nje ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam baada ya mtuhumiwa
wa kutishia mauaji ya mwenzao aliyefikishwa kituoni hapo jana kudaiwa
kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo walilipinga.Watu
wenye ulemavu wa ngozi (albino), jana walizua tafrani Kituo cha Polisi
Buguruni, wakipinga dhamana kwa mshtakiwa, Ombeni Swai (34), mkazi wa
Tabata Matumbi anayekabiliwa na kesi ya kutoa vitisho vya kumuua
mwenzao.
Tafrani
hiyo ilianzia katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni baada ya mshtakiwa
huyo kusomewa mashtaka na Karani wa Mahakama, Edwin Wandanda na kisha
Hakimu Mfawidhi, Benjamin Mwakasonda aliyekuwa akiisikiliza kusema
dhamana ya mshtakiwa iko wazi.
Polisi
wa Kituo cha Bungurini wakiwa na silaha zinazodaiwa kutumiwa
kuwatawanya watu wenye ulemavu wa ngozi kituoni hapo wakati wakizuia
gari ilikuwa imebeba mtu anayetuhumiwa kumuua Albino baada ya
kufunguliwa mashitika katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni.
Ingawa
mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, albino waliokuwapo
mahakamani hapo hawakufurahishwa na kitendo cha kuwapo kwa nafasi ya
dhamana kwa mshtakiwa wakidai kwamba ameshatoa vitisho vya mauaji dhidi
yao. Baada ya kulalamika mahakamani
hapo waliandamana hadi kituoni hapo ambako mshtakiwa alikuwa amepelekwa
hali iliyosababisha polisi kituoni hapo kutumia risasi za baridi
kuwatawanya na kusababisha taharuki kwa wafanyabiashara na wakazi wa
eneo hilo.
Mwandishi wetu alishuhudia baadhi ya watu wakiwa wamesimama, wengine wakikimbia ovyo huku polisi wakiwa silaha.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Ilala, Mariam Nzuki alisema vurugu hizo ziliongezeka baada ya kundi la vijana wa sokoni kuungana nao.
Alisema baada ya polisi kuona hivyo, walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya na kumpeleka mtuhumiwa katika Mahabusu ya Segerea.
Hati ya mashtaka Mshtakiwa
anadaiwa kuwa Agosti 16, mwaka huu maeneo ya Buguruni kwa Mkanda
alitishia kuua kwa maneno watu wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo
hayo.
Hati hiyo inadai kuwa mshtakiwa alimtishia kwa maneno mlalamikaji, Mwinyiusi Issa kuwa atamuua kama anavyoua albino. Mengi ajitolea Wakati
hayo yakitokea, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi
amejitolea kuwasomesha watoto wawili wa albino Suzan Mungi, aliyekatwa
kiganja cha mkono na watu wasiojulikana wilayani Igunga mkoani Tabora.
Akizungumza
jana, Mengi alisema amesikitishwa na tukio hilo ambalo mume wa Suzan,
Mapambo Mashili aliuawa wakati akijaribu kumtetea ili asifanyiwe ukatili
huo. “Sina mamlaka ya kuwaadhibiti
wahalifu hawa lakini naahidi kutoa Sh10 milioni kwa mtu atakayewezesha
kukamatwa kwao, Serikali inapaswa kuwashughulikia wahusika wote yaani
wanaofanya ukatili huo, wanaohitaji viungo hivyo na waganga wa
kienyeji,” alisema.Crdt DjSek Blog
on Wednesday, August 20, 2014
Post a Comment