Pichani ni baadhi ya Daktari wakiwa wamembeba mgonjwa wa EBORA picha kwa hisani ya Mtandao.
Na Hannah Mayige, wa Chuo Kikuu Huria, OUT
TISHIO
la ugonjwa wa Ebola unaoendelea kuuwa mamia ya watu Afrika Magharibi,
umezua wasiwasi mkubwa kwa nchi za Afrika na dunia
nzima kwa ujumla na kutakiwa watanzania kuchukua tahadhari kubwa kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.
nzima kwa ujumla na kutakiwa watanzania kuchukua tahadhari kubwa kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.
Lazima Serikali na wananchi wazingatie masharti na tahadhari
inayotolewa kimataifa kuudhibiti ugonjwa na utayari wake wa kupambana
nao.
Ugonjwa wa Ebola, umekuwa tishio kubwa kwa uhai na ustawi wa mataifa
mbalimbali yakiwemo ya Afrika Mashariki ambako Tanzania ni mojawapo.
Mpaka sasa, nchi zilizoathirika na ugonjwa huo ni pamoja na Cameroon, Liberia na Nigeria ambapo tayari zaidi ya
watu 1,000 wamepoteza maisha.
watu 1,000 wamepoteza maisha.
Eneo la Afrika mashariki, kuna taarifa kuwa hivi karibuni alipatikana
mgonjwa wa Ebola katika nchi ya Rwanda na kwamba miaka ya nyuma
milipuko iliwahi kutokea nchini Uganda.
Ebola ni ugonjwa ambao mpaka sasa hauna tiba wala chanjo,
ambapo huambukiza kwa njia ya hewa au majimaji yatokayo
mwilini kama mate , jasho, damu na kwamba mgonjwa akigusana na mtu asiye na virusi hivyo basi anaambukizwa.
ambapo huambukiza kwa njia ya hewa au majimaji yatokayo
mwilini kama mate , jasho, damu na kwamba mgonjwa akigusana na mtu asiye na virusi hivyo basi anaambukizwa.
Shirika la Afya Duniani [WHO] limetahadharisha nchi
mbalimbali hasa Afrika kuchukua tahadhari kubwa, mfano hivi
karibuni ndege za shirika la Kenya lilishauriwa kutoendelea na
safari zake za Afrika Magharibi kwa kuhofia baadhi yaabiria wake
kuhamisha virusi vya Ebola na kusambaza katika eneo la Afrika
Mashariki. Kenya ni mojawapo ya nchi za Afrika mashariki zenye safari nyingi za ndege kuelekea mataifambalimbali.
Kutokana
na wito huo wa WHO, tayari Korea imesitisha safari zake za ndege
kwenda Kenya kwa tahadhari ya kudhibiti usambaaji wa Ebola.
Kwa kuwa ugonjwa huo unaambukiza kwa njia ya hewa pia na
majimaji yatokayo mwilini hata madaktari na wauguzi wanalazimika
kuwa na mavazi maalum ambayo yanafunika mwili mzima, kwani hawatakiwi kugusana kwa namna yeyote ile.
Msimamizi wa Vituo vya Afya mipakani Tanzania, Dk. Khalid Massa,
anasema vifaa hivyo ni pamoja na magauni, aproni, buti, gloves na
vifaa maalum vya kuziba pua na mdomo. “Wahudumu wanatakiwa
kuvaa vifaa hivyo kujikinga na maambukizi na tayari vifaa
20,000 vimepokelewa na kusambazwa katika maeneo yaliyoainishwa,” anasema
Dk. Massa.
Dk.
Massa, anasema kwa kushirikiana na maofisa uhamiaji wamejikita zaidi
kuchunguza wasafiri wa ndege hasa wanaotokea Afrika Magharibi.
Naye, Mtaalamu wa Kudhibiti magonjwa ya mlipuko Dk. Vida
Makundi,anawaasa wananchi kuripoti mapema katika vituo vya afya au kwa
viongozi wa serikali za mitaaa endapo watakuwa na dalili za ugonjwa
huo.
Anazitaja
dalili kubwa ambazo zimeelezwa na Shirika la Afya duniani ni
pamoja na kuumwa sana kichwa , kupata homa kali, na hatimaye
kutokwa na damu katika maeneo yenye uwazi, kama vile mdomoni, ngozi,
masikioni na sehemu za siri.
Ebola
imesababisha hofu na tafrani kubwa kwa nchi hasa zinazoendelea kwa
kuua watu bila kupata tiba ikiwa ni pamoja na madaktari na udhoofisha
hali ya uchumi kutokana na shughuli nyingi za kusafiri na
zinazokutanisha watu kusitishwa.
zinazokutanisha watu kusitishwa.
Shughuli
za biashara za kimataifa pia zinaendelea kutetereka kuogopa
maambukizi ya virusi vya Ebola hasa wananchi katika nchi zenye
ugonjwa huo kuogopana wenyewe kwa wenyewe.
Mfano,
huko Cameroun, kuna mtu alikutwa amekufa barabarani hakuna mtu
aliyethubutu kumsogelea mpaka walipokuja madaktari ambao walivalia
rasmi kuhakikisha hakuna maambukizimapya kwa watu wengine.
Hapa
Tanzania, tayari serikali kupitia viongozi mbalimbali akiwemo Makamu
wa Rais Mohamed Ali Bilal , Waziri wa Afya Dk. Seif Rashid na baadhi
ya wakuu wa mikoa ya Manyara, Dar es Salaam na Mbeya
wamewataka wananchi kuwa waangalifu na wageni wasio wajua na kuwa
tahadharisha kwenda hospitali mara wanapoona wana dalili zisizo
za kawaida au zinazoashiria ugonjwa
wa Ebola.
za kawaida au zinazoashiria ugonjwa
wa Ebola.
Kulingana
na tamko la serikali , Ebola bado haijaingia nchini lakini usemi wa
Kiswahili usemao ‘ ukiona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji’.
Kwa
upande wa kutenga maeneo maalum ya kushughulikia wagonjwa wa Ebola,
serikali imetenga maeneo mawili kwa Dare s Salaam, Temeke na Hospitali
ya Taifa Muhimbili.
Waziri
wa afya DK. Seif Rashid anasema tayari wauguzi na madaktari
wanapatiwa elimu kuhusiana na kuudhibiti ugonjwa wa Ebola kabla
haujaingia nchini, elimu hiyo inatolewa katika hospitali zote .
Nao,
wananchi kwa nyakati tofauti wameendelea kumlilia mungu kwa mlipuko wa
magonjwa hapa barani Afrika. “Mara ukimwi, mara Dengue mara Ebola yote
hakuna tiba,” analalamika mmoja wa wananchi Kasian Komba mkazi
wa Songea.
Kutokana
na taarifa za baadhi ya wananchi wa Liberia kuvamia kituo kilichotengwa
kuhudumia wagonjwa wa Ebola na kupora magodoro, vifaa na wagonjwa
kutawanyika, ni taarifa mbaya na huenda imetokana na kukosa elimu
ya ugonjwa huo.
Kwakuwa elimu ni muhimu, ni vyema serikali hapa nchini ikatumia fursa
hii kuelimisha umma kwa kutumia mikutano ya hadhara, Sanaa za
maonesho, mabango, vyombo vya habari kama mitandao ya kijamii, redio, televisheni, magazeti na vipeperushi ili jamii ipate uelewa.
maonesho, mabango, vyombo vya habari kama mitandao ya kijamii, redio, televisheni, magazeti na vipeperushi ili jamii ipate uelewa.
Makala hii imeandikwa na Hannah Mayige, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania – OUT. Anapatikana kwa E-mail hannahmayige@gmail.com
Post a Comment