Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne
Neema Steven Mtwanga(16) anayesoma katika shule ya sekondari Naboti
Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa
insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo
kusini mwa Afrika(SADC).
Rais
Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa
mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii
wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo mwanafunzi huyo aliandika
insha inayohusu mabadiliko ya tabia nchi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu
na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda
mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika
katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe leo.
Katikati ji mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe. Picha na Freddy Maro
Post a Comment