Tukio hilo la kusikitisha lilijiri
juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo mwanamke aliyetajwa kwa jina
moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala huo uliotokea nyumbani kwake
maeneo ya Mtaa wa Ndege, Msamvu mjini hapa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
walidai kwamba, siku ya tukio, Fatuma alimshutumu Mwajuma kuwa amekuwa
akimwambia mumewe maneno ya umbeya ili kuwatenganisha.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila baada ya siku tatu anakuja kwenye nyumba hii kumsalimia mama yake mdogo.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila baada ya siku tatu anakuja kwenye nyumba hii kumsalimia mama yake mdogo.
“Juzi Fatuma aligombana sana na mumewe na chanzo cha ugomvi huo ilidaiwa kuna mambo mwanaume huyo aliambiwa na Mwajuma.
“Mwajuma alipofika kwa mama yake mdogo ndipo Fatuma akamkwida na kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe mambo ya umbeya?
“Mwajuma alipofika kwa mama yake mdogo ndipo Fatuma akamkwida na kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe mambo ya umbeya?
“Mabishano yalishika kasi na mwishowe
walipigana. Fatuma alipoona amezidiwa, akaingia jikoni na kuipua sufuria
la maharage yaliyokuwa yakichemka na kumwagia Mwajuma mwilini,” alisema
mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Akizungumza na paparazi, mama mdogo wa
Mwajuma alisema: “Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye kijiji kimoja
Turiani. Ni kweli alimmwagia Mwajuma maharage ya moto mwilini.“Fatuma
alikuwa anamshutumu mwanangu kumchonganisha na mumewe ndipo walipoanza
kupigana.
“Fatuma alipoona kazidiwa aliingia
jikoni akaipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka wna kummwagia
mwanangu mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.”
Mume wa Mwajuma, Peter Muhanda alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo na kwamba alitoa taarifa polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa.”
Mume wa Mwajuma, Peter Muhanda alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo na kwamba alitoa taarifa polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa.”
Post a Comment