Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Aunt Ezekiel Anaswa na Mume Wa Mtu......Ni siku chache baada ya kuahidi kumpa penzi, Madai ya kulala pamoja hotelini yaenea kila kona

Staa wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa na vituko, Aunt Ezekiel (katikati) akiwa karibu na dansa wa Wasafi Classic, Moses Yobo.
******
Staa wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa na vituko, Aunt Ezekiel amenaswa live akijivinjari na mume wa mtu.

Aunt alinaswa akiwa na mnenguaji wa Wasafi Classic, Moses Yobo anayepiga mzigo chini ya Nasib Abdul ‘Diamond’ katika shoo ya Fiesta iliyofanyika jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba, wikiendi iliyopita.
Wiki chache zilizopita, habari ya Aunt kufanyiwa vurugu nyumbani kwa Wema na mke wa Yobo aliyekuwa na timu yake ilitawala katika mitandao ya kibongo.

Baada ya habari hiyo , Aunt aliibuka na kusema kuwa, hana uhusiano wa kimapenzi na Yobo lakini kwa sababu amezushiwa, akaahidi kujiweka karibu na kumfanyia mitego ili atoke naye kweli ndipo afanyiwe vurugu ya halali.
Kuonekana akiwa naye jijini Mwanza, tena kwa ukaribu kama wapenzi huku wawili hao kila mmoja akiwa hana mpenzi wake anayetambulika, kulitafsiri kuwa Aunt ameamua kukinukisha.
Habari ambazo hazijathibitishwa kutoka kwa watu wa karibu na Aunt, zinasema kuwa, usiku huo baada ya shoo, wawili hao walilala pamoja katika hoteli ambayo haijajulikana.

Mwandishi wetu baada ya kuona hali na ukaribu huo alimfuata Aunt ili kujua kama kweli ameamua kutekeleza azma aliyoitangaza, lakini akaruka kimanga.
“Nimeamua kukaa na Yobo karibu ili kuwazingua wasanii ambao baada ya kuniona wakawa wananitania eti mimi mkewe kutokana na taarifa za magazeti zilizoripotiwa hivi karibuni, ila ukweli mwenyewe unaona tupo hapa na Wema (Sepetu) na watu wengine na kimsingi hakuna kitu kibaya kinachoendelea kati yetu,” alisema Aunt.
Chanzo: Risasi Mchanganyiko/ Gpl
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top