Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesisitiza kuwa vitambulisho vya taifa
vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), havitatumika
kupiga kura katika uchaguzi mkuu, isipokuwa kadi zitakazotolewa na tume
hiyo.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi, Julius Mallaba alifafanua jana jijini Dar es Salaam kwamba
ni makosa kudhani kuwa vitambulisho vinavyotolewa na Nida, vinaweza
kutumika kupiga kura.
“Haiwezekani
kabisa…tunaomba watu waelewe kuwa kadi za kupiga kura na vitambulisho
vya uraia ni vitu viwili tofauti. Vitambulisho vya taifa siyo mbadala wa
kadi za kupiga kura,” alisisitiza.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi huyo, kwa hali ilivyo utoaji wa vitambulisho vya
taifa kwa nchi nzima, utachukua muda mrefu na kwamba hata baada ya
uchaguzi ulioagizwa kisheria kupita, watu wengi watakuwa hawajapata
vitambulisho hivyo.
Mkurugenzi
alitoa ufafanuzi huo, kutokana na kile alichosema ni kutokana na kuwepo
taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba mtu asiye na kadi ya
kupiga kura, anaweza kutumia kitambulisho cha uraia kupiga kura.
Alisema
wakati uandikishaji wa NEC unafanyika kwa muda maalum ili kuwahi
upigaji wa kura ya maoni na uchaguzi mkuu, uandikishaji wa Nida hauna
muda maalumu.
“NEC
ina mchakato mfupi wa ukusanyaji wa taarifa za watu wanaoandikishwa na
kadi za mpiga kura zinatolewa papo hapo kituoni baada ya ujazaji wa
fomu,” alisema.
Kwa upande wa Nida, mchakato wa ukusanyaji wa taarifa una utaratibu mrefu kutokana na wahusika wa zoezi hilo kuwa wengi.
Akielezea zaidi alisema namba ya kadi inayotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi ni ya kipekee kwa mtu anayeandikishwa.
Nida
inaweza kutoa namba zaidi ya moja endapo itabidi kutoa kitambulisho
kingine kwa mtu huyo huyo, kutokana na kitambulisho cha awali kupotea au
kuharibika.
Mallaba
alisema hata kama vitambulisho vya uraia vingekuwa tayari, bado tume
ingetakiwa kuandaa daftari kwa kuwa vitambulisho vya uraia huwa
haviainishi mtu ni mpiga kura wa eneo gani.
Alifafanua
kuwa kama wananchi wote wangekuwa na vitambulisho vya taifa, kitu
ambacho kingefanyika ni kwa tume kununua kifaa kinachoweza kusoma
kitambulisho na kupata taarifa za mhusika na kumpangia mhusika sehemu
yake ya kupigia kura.
Alisema
hakuna nchi katika bara la Afrika, inayotumia kitambulisho cha taifa
moja kwa moja katika kupiga kura, isipokuwa hutumika kurahisisha
utaratibu wa kuandaa daftari la kudumu la wapiga kura.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji
mstaafu Damian Lubuva alisema uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa
upande mmoja na vitambulisho vya wapiga kura kwa upande mwingine ni
shughuli tofauti, lakini zinazohusiana kwa karibu na pia zinazohusu
wananchi
Post a Comment