Memba wa Kundi la Tip Top Connection , Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ akipozi kimahaba na mwanamuziki Mwanaisha Abdallah ‘Nyota Ndogo’.
Memba wa Kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ na mwanamuziki wa nchini Kenya, Mwanaisha Abdallah ‘Nyota Ndogo’ wamenaswa laivu wakiwa kwenye pozi la mahaba niue.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kutoka
nchini humo, wawili hao walikuwa wakijiachia nyumbani kwa Nyota Ndogo
huku kukiwa na madai mazito kuwa eti wanapika na kupakuwa.
Ilidaiwa kwamba Tunda Man anapokwenda
Kenya huwa anafikia nyumbani kwa Nyota Ndogo. “Wasanii wengi wanakuja
Kenya wanajifanya kuja kufanya shoo kumbe wanawafuata wanawake zao ila
mimi namsihi Tunda Man ajiangalie, yasije yakamkuta kama ya wasanii
wengine walivyopewa masaa ishirini na nne wasikanyage Kenya tena,”
kilisema chanzo hicho.
Baada
ya kupata maelezo hayo, paparazi alimvutia waya Tunda Man na kumpa
hongera ya kummiliki Nyota Ndogo ambapo alikuja juu na kudai kuwa
anahisi anataka kuchafuliwa.
“Kaka nadhani unajua kuwa nina mke na sijawahi kupata skendo kubwa kama hiyo, Nyota Ndogo namheshimu kama dada yangu na sijawahi hata kufikiria kumtongoza please achana na hiyo habari,” alijitetea Tunda Man bila kujua tuna picha zao za mahaba.

Post a Comment