Mamlaka
ya anga nchini India inachunguza tukio la hatari lililotokea Agosti 8,
baada ya ndege ya Jet Airways Boeing 777-300 iliposhuka angani kwa zaidi
ya futi 5000 (mita 1500) kutoka kwenye urefu waliopangiwa kuruka baada
ya rubani wake kusinzia.
Tukio hilo lilitokea wakati ndege hiyo ikifanya safari kutoka Mumbai, India kwenda Brussels, Ubelgiji.
Times of
India imeripoti kuwa rubani aliyekuwa akiongoza ndege hiyo alipumzika
kidogo, mapumziko ambayo kwa viwango vya kimataifa huitwa ‘controlled
rest’ kwa zile ndege za masafa marefu. Safari ya ndege kutoka Mumbai
hadi Brussels ni masaa 9.
Rubani
msaidizi alitakiwa kuchukua majukumu yote ya kuongoza ndege kwa wakati
huo, lakini inadaiwa rubani huyo wa kike alisema naye alikuwa busy na
tablet ya ndege hivyo hakugundua ndege ilipoanza kushuka kutoka kwenye
urefu wa futi 34,000 iliyotakiwa kuruka wakati wanapita Uturuki.
Kwa
bahati nzuri waongozaji wa anga wa Uturuki waligundua kuwa ndege hiyo
iliyokuwa katika anga lao imeshuka kwenye urefu (altitude) ambao
umepangwa kwaajili ya ndege nyingine, na kumtaarifu rubani msaidizi
arudi kwenye urefu waliopangiwa.
Marubani wote wawili wa ndege hiyo wamesimamishwa kupisha uchunguzi .
Source: Aljazeera
Post a Comment