Taswira baada ya ajali hiyo.
STAA wa filamu za Kibongo, anayepatia zaidi kuigiza kama Mchungaji,
Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ amepata ajali baada ya gari lake aina ya
Toyota Creasta kugongwa na gari lingine leo mchana katikati ya Boko na
Bunju jijini Dar es Salaam.
Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa zaidi ya magari hayo mawili kuharibika.
Kwa mujibu wa Pastor Myamba, dereva aliyekuwa akiendesha gari
lililogonga gari lake alitokomea na kuacha gari lake eneo la tukio baada
ya kugundua kuwa ndiye aliyekuwa na makosa.
Magari yote mawili yamevutwa na 'breakdown' kisha kupelekwa kituo cha polisi Tegeta.
Post a Comment