Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Tabora Bw.Kansa
Mbaruku na Mwenyekiti wa kamati ya Sheria na haki za binadamu kanda ya
magharibi ambaye pia ni Mwanasheria mkongwe Bw.Mussa Kwikima wametangaza
kujiuzulu rasmi leo hii mbele ya waandishi wa habari kufuatia madai ya
kuendelea kukiukwa kwa maadili ya viongozi kuanzia ngazi ya juu ambao
wamekuwa wakivunja katiba kwa maslahi yao binafsi.
Kujivua madaraka kwa
viongozi hao wawili huenda ikawa pigo kubwa kwa Chadema kanda ya
Magharibi baada ya mmoja kati ya makada mahili wa chama hicho wilaya ya
Igunga Bw.Anuar Kashaga kuondoka Chadema na kujiunga na Chama cha
Mapinduzi katika siku za hivi karibuni.
Hatua ya kuachia ngazi kwa
viongozi hao imedaiwa kuwa kuna siri nzito ya wimbi la ubaguzi wa
kikabila,kikanda na hata kidini ambayo bado viongozi hao wamekuwa na
kigugumizi kuweka hadharani.
NA KAPIPI J
Post a Comment